Loading...

Makonda: Simwogopi Magufuli

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amedai kwamba hafanyi kazi kwa kumwogopi Rais John Magufuli, anaandika Regina Mkonde.
“Nafanya kazi zangu ipasavyo na si kwa woga wa rais. Namuomba Mungu anisaidie nisitumie cheo na madaraka yangu kugandamiza wengine,” amesema Makonda.
Hata hivyo, Makonda amejidhihirisha kuwa kiongozi mbabe. Mwaka juzi alimvamia Jaji Joseph Warioba, katika mdahalo wa katiba Mpya, jijini Dar es Salaam, akamrushia makonde na mdahalo ukavunjika.
Baada ya hapo aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni. Desemba mwaka jana, alitumia mamlaka yake vibaya kwa kuamuru polisi wamkamate Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, baada ya wawili hao kutofautiana kauli wakiwa kwenye usuluhishi wa mgogo wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Tooku na menejimenti, jijini Dar es Salaam.
Makonda alitoa kauli hiyo jana wakati akikabidhiwa ofisi na Said Mecky Sadick, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Sadick amehamishiwa mkoani Kilimanjaro kushika wadhifa huo.
Kwenye makabidhiano hayo Makonda amevitaka vyama vya upinzani kuachana na siasa za ubaguzi na kwamba, wanapaswa kufanya siasa wakati uchaguzi utapokaribia.
“Huu si wakati wa kuendekeza siasa za kibaguzi, si wakati wa propaganda za kuchafuana, tufanye kazi. Wananchi wanahitaji kuona mabadiliko kama mlivyokuwa mnajinadi kwenye kampeni za uchaguzi, subiri mwanzoni mwa waka 2020 ndiyo muanze siasa.
“Nitafanya kazi kwa kuzingatia kanuni, katiba na ilani ya CCM katika kutatua changamoto za Jiji la Dar es Salaam,” amesema Makonda.
Akikabidhi ofisi hiyo, Sadick alimwambia Makonda kwamba jiji hilo haliongozwi na upinzani kama ambavyo inaelezwa na vyama hivyo.
“Dar es Salaam haijakamatwa na upinzani, bali ni mameya na wabunge ndiyo wengi. Hii haimaanisha kwamba jiji linashikwa na upinzani,” amesema Sadick.
Kwenye makabidhiano hayo Sadick amesema, atakapokwenda kuanza kazi Mkoa wa Kilimanjaro hatapambana na vyama vya siasa bali atashughulikia maendeleo.
“Siendi kupambana na vyama vya siasa mkoani Kilimanjaro, ninakwenda kusimamia maendeleo, awe kiongozi wa CCM au Chadema sawa, sote tuna nia ya kujenga nyumba moja,” amesema.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top