Loading...

BREAKING NEWS NI ZAIDI YA AIBU NI LAANA CHAFU ALIOYOFANYA MSHAURI WA RAIS SHEIN KUTWA AKILA ARODA BINTI MDOGO WA MIAKA 20 HILI NI TUKIO LA PILI TENA ZANZIBAR....

Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar (katikati) akipokea ripoti kutoka kwa Dadi Faki Dadi aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
SERIKALI ya Dk. Ali Mohammed Shein imezama kwenye aibu, ni baada ya mshauri wake Dadi Faki Dadi kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na mwanaye, anaandika Pendo Omary.
Faki alikuwa Mkuu Mkoa wa Kaskazini Pemba lakini baada ya kukosa nafasi hiyo katika ngwe ya pili ya Dk. Shein, aliteuliwa kushika nafasi hiyo ya ushahuri kwa rais hususan masuala ya yanayohusu Pemba.
Mshauri huyo amekamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na mtoto wake wa kambo (mtoto wa mkewe) mwenye umri wa miaka 21.
Mwanasiasa huyo maarufu visiwani humo alikamatwa mbele ya mkewe na baadhi ya wanafamilia juzi katika nyumba ya wageni ya Executive, jirani na Makao Makuu ya Uhamiaji Zanzibar, eneo la Kilimani mjini Unguja na kupelekwa katika kituo cha Polisi Mwembemadema.
Mkadam Khamis, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi amethibitisha kushikiliwa kwa Dadi na polisi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.
“Tunaendelea kufanya uchunguzi. Iwapo tutabaini ametenda kosa tutampeleka katika vyombo vya sheria,” amesema Khamis.
Aidha, picha za video ambazo zinaendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii zinamuonesha Dadi akishambuliwa kwa maneno makali kutoka kwa mkewe na watu waliomkamata.

HABARI YA HIWVI PUNDE: MTOTO WA MIAKA MINNE ATOA SIRI NZITO NA MKASA WOTE WA TUKIO LA MAUWAJI YA ANETH MSUYA MSIKILIZE HAPA MTOTO HUYU HUU NI ZAIDI YA UNYAMA ALIOFANYIWA DADA HUYU....


             
May 26 kulitokea mauaji ya kutisha ya kukatwa mapanga kwa mwanadada Aneth ambaye ni ndugu wa Tajiri mmoja ambaye naye aliuliwa kwa kupigwa risasi. Aneth amepigwa mapaga na watu wasiojulika na kukimbia. Jirani wa Anetha pia mfanyakazi mwenzake anafafanua vizuri,
     “Yaani Aneth hata siamini, jana tulikua nae kazini, kaondoka kufika nyumbani akakuta housgal katoroka, akapiga simu kwa mwenzetu akamueleza kwamba leo hatokuja ili angalie logistics. 
 Mtoto wake ana miaka minne ndio alipo hojiwa alisema hivi jana walikuja watu watano weusi, wakavunja mlango ni majira ya mama saa tatu usiku, akakimbia chumbani, walipoingia wakamkuta mtoto wakauliza mama huko wapi akasema chumbani, wakamfuata huko mtoto hajui kilichoendelea. hadi  asubuhi school bus ilipokuja alijaribu kutoka akashindwa na mwishowe iliondoka.
Anafafanua: Baada ya kuona mama yake haamki ndipo alipotoka kwa jirani na kuwaita. Majirani walikwenda na kukuta Aneth akiwa amechinjwa na akiwa uchi (seems walimbaka) kisu kipo hapohapo na hawajaiba kitu.

Inasemekana alikuwa anafyatilia sana kes ya marehem kaka ake Msuya yule bilionea wa arusha aliuawa kwa kupigwa risasi

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI SASA HASHIKIKI TENA HII MOJA YA TUKIO LA KIHISTORIA KATIKA UTAWALA WAKE MPAKA SASA AMUA WAZIWAZI KUPINGANA NA UKWELI WA JAMBO HILI NA KUAMUA HAYA....

anayepingana na ukweli kwamba ‘Wazee ni hazina ya Taifa la Tanzania’ lakini acha  ukweli uzungumzwe, kwani ‘kubebana’ na‘kuleana’ kumetufikisha hapa tulipo.

Tabia iliyojengwa na wazee ya kufanya kazi kwa mazoea huku waking’ang’ania madaraka kunalifanya taifa kupiga ‘mark time’ badala ya kusonga mbele; tafiti zinaonesha asilimia kubwa ya vijana wasomi wapo mitaani na hawana ajira kutokana na nafasi hizo kukaliwa na wazee, tena ambao hawana elimu sawa na vijana wasomi ambao wanasota mitaani.

magufuliJambo hili linamfanya Rais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuamua kufanya kazi na vijana katika serikali yake kwani amegundua licha ya vijana wachapakazi kutopendwa na baadhi ya watu, ni wachapakazi na watamsaidia kulipeleka taifa katika maendeleo anayoyatamani, kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawapendi rushwa.

“Nimegundua vijana wengi hawapendi rushwa, hivyo nitaongeza vijana kila nikiteua kwa kuwa niliowaweka naona matunda ya kazi zao, najua watu wanawachukia sana ila nitawaongeza. Palipo na vijana nimeona mambo yanaenda na kuna mabadiliko. Wazee ndio tumelifikisha taifa hili hapa, hakuna asiyejua kuwa Tanzania ilichakaa kila mahala”.

mbarawaNi wazi hivi sasa wazee wamekalia kuti kavu katika Serikali ya Awamu ya Tano kwani Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amefuata nyayo za Rais Magufuli katika ‘operesheni fukuza wazee’ baada ya kutamka wazi kwamba wakati umefika kwa wazee wanaofanya kazi katika Kampuni ya Simu ya TTCL kuwaachia Vijana kwa sababu wazee wamekua watu wa kuzungumza zaidi kuliko vitendo kwani Sekta ya Mawasiliano hivi sasa ina ushindani mkubwa.

BREAKING NEWS: NI TUKIO AMBALO HALIKUWA LA KAWAIDA TENA TABATA DIWANI CHADEMA MFANYIA UKASKI WA AJABU NDANI YA MAHAKAMA DIWANI HUYU WA CCM....

Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu
PATRICK Asenga Diwani wa Kata ya Tabata (Chadema) ameshinda kesi ya uchaguzi aliyofunguliwa na Sudi Kasim aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, anaandika Faki Sosi.
Kasim alifungua kesi hiyo akipinga matokeo ya kiti hicho katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana kwa madai kwamba haukuwa huru na haki.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo leo katika Mahakama hiyo, Frank Moshi hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri hilo amesema, anatupilia mbali kesi hiyo kwasababu mdai ameshindwa kuthibitisha malalamiko yake.
Miongoni mwa vitu alivyoshindwa kuthibitisha ni pamoja na uwepo wa vurugu katika kituo cha majumuisho ya kuhesabia kura ambapo hata wakala wake ameshindwa kuthibitisha hilo katika ushahidi wake.
Kutokana na hali hiyo, hakimu alisema kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki na kwamba Asenga ni diwani halali wa kata ya Tabata na atalipwa gharama ya 30 milioni kama fidia ya kesi hiyo.
Akizungumza nje ya mahakama, diwani Asenga amewashukuru wananchi wake kwa ushirikiano waliouonesha na kuahidi kuwa gharama za kesi atakazolipwa ataziingiza katika miradi ya maendeleo ya kata hiyo.
Amesema kuwa gharama hizo   nakwamba atawasilisha madai ya fedha hizo mapema ili aweze kulipwa.
“Nashukuru wananchi wangu kwani nipo pamoja nao,mahakama imetenda haki.Hii kesi ilinipotezea muda wa kuwatumikia ,lakini kwasasa nipo huru na nipo tayari kuchapa kazi “amesema
Katika kesi hiyo,wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ilala.
Katika kesi hiyo, Kasim aliiomba mahakama hiyo itenguwe matokeo ya uchaguzi kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza na kwamba imtangaze yeye kama mshindi.

HABARI YA HIVI PUNDE: KUTOKA BUNGENI KIMENUKA TENA BUNGENI JIONI HII JUMA NKAMIA AZUA MTAFARUKU MKUBWA NDANI YA MBUNGE BAADA KUWATUSI UKAWA MATUSI YA AJABU MNO SHUDIA TUKIO HILI LILOZUA MTIFUANO MZITO NDANI YA BUNGE....

Kanuni inayozuia lugha ya kuudhi bungeni ni kiinimacho kwani mbunge wa upinzani akitoa lugha inayokera, mbunge wa CCM ataomba mwongozo kwa Spika na mara akijibiwa atasimama mbunge wa CCM na kutumia lugha hiyo hiyo iliyoombewa mwongozo.

Jana Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) aliporomosha lugha za kuudhi baada ya kuwaambia wabunge wa upinzani waliokuwa wakishangilia kuwa wanasura mbaya hadi wanatamani kutapika.

Akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa mwaka 2016/17, Nkamia alionyesha kukerwa na hotuba ya upinzani kuhusu wizara hiyo kwenye sehemu iliyozungumzia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Nkamia alisema uchaguzi umepita na mshindi alipatikana ambaye ni CCM na aliufananisha uchaguzi na mpira kwamba unapoisha uwanjani mtu hawezi kulalamika nje.

“Uchaguzi umeisha, leo mtu anasimama hapa anasema ‘ooh tuliibiwa kura’ mlikuwa wapi wakati mnaibiwa kura?”alihoji na kuwataka wapinzani watafute sababu kwa nini walishindwa na si vinginevyo.

"Wanajua mchezaji mmoja akiumia katika timu unachukua mwingine kwenye timu ile ile lakini inakuwaje unachukua mchezaji kutoka upinzani? Kwa hiyo niwaombe tu muwe mnatafakari kwanza,” alisema.

Hali hiyo iliibua kelele na minong’ono kutoka kwa wapinzani, jambo ambalo lilimlazimu Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwataka wabunge huku akiwataja majina watulie ili mbunge huyo amalizie mchango wake.

Nkamia aliendelea, “We nyosha midomo, fanya nini lakini that is the truth (huo ndiyo ukweli). Utaongea sana na utapiga kelele sana lakini ukweli ndio huo na umekuingia vizuri.

"Mimi kelele wala hazinisumbui. Mimi nataka niwashauri kama wakati ujao mnataka kuwa chama kizuri anzeni kutafuta wachezaji wenu,” alisema.

“Nyie pigeni kelele lakini ukweli ndio huo, wenye akili wanajua na wapiga kelele wanajua na najua limewaingia vizuri sana.”

Kijembe hiki kiliwalenga Ukawa ambao katika uchaguzi mkuu uliopita walimteua aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa. Ukawa walimteua Lowasa baada ya kuitema na kuihama CCM ambapo alipambana na John Magufuli (CCM) aliyeshinda.

Nkamia akionekana kumlenga mbunge fulani ambaye hakumtaja jina alisema, “We piga kelele, kwanza meno yako yameoza.”

Kwa kuzingatia kanuni, lugha hiyo ni ya kuudhi lakini Dk Tulia asisitiza Nkamia amalizie kuchangia ambapo alitoa mfano wa mwandishi wa vitabu Bernard Taper aliyewahi kusema kwamba kuna watu wakiamka asubuhi wakijiangalia kwenye kioo wanatamani kutapika.

“Sasa nyie mnaoshangilia humu mna sura mbaya na mnatamani kutapika,” alisema Nkamia

BREAKING NEWS: TUKIO LA AINA YAKE JESHI LA POLISI ZANZIBAR LAFANYA KWA MAALIM SEIFU IKUMBUKWE LEO NDIO MAALIM SEIF ALITAKIWA KUHOJIWA NA POLISI SASA SIKIA HICHI ALICHOKIANDIKA DCP MSANGI KWA MAALIM....



Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad
Katika barua yake kwa Maalim Seif iliyosainiwa na DCP Salum Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, haikutaja ni lini mahojiano hayo yatafanyika lakini imesema, “Tutakujulisha mapema siku ya mahojiano itakayofuata mara baada ya kukamilisha taratibu”.


By Hassan Ali, Mwananchi hali@mwananchi.co.tz
Zanzibar. Jeshi la Polisi Zanzibar limeahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kwa sababu zilizoelezwa kuwa nje ya uwezo wake.
Katika barua yake kwa Maalim Seif iliyosainiwa na DCP Salum Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, haikutaja ni lini mahojiano hayo yatafanyika lakini imesema, “Tutakujulisha mapema siku ya mahojiano itakayofuata mara baada ya kukamilisha taratibu”.
Barua hiyo ya Mei 26 imenukuu barua ya awali ya Mei 22, 2016 iliyomuita mwanasiasa huyo makao makuu ya polisi Zanzibar kwa mahojiano kuhusu, “masuala mbalimbali yanayohusu ulinzi na usalama wa visiwa hivi.”
Kutokana na hatua hiyo, Maalim Seif aliyetarajiwa kuwasili saa 3 asubuhi Zanzibar kutoka Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa aliahirisha safari hiyo na atawasili Saa 10 za jioni kwa ajili ya maandalizi ya ziara yake ya kichama kuanzia kesho katika wilaya saba za Unguja.

BREAKING NEWS: MBUNGE ASIEKAUKIWA MANENO BUNGENI BASHE BAADA YA KUWAITA WANAFIKI CCM AZIDI KUISASAMBUA CCM MSILIZE TENA HAPA....

BASHE

Mbunge wa Nzega Mjini Hussen Bashe amesema Bungeni kwamba wabunge na serikali nzima wana wajibu wa kutatua kero za wananchi na wakishindwa kufanya hivyo hakuna haja ya kuendelea kuwa madarakani.

Bashe ameyasema hayo kwa kuwakumbusha wabunge hotuba ya Rais wa awamu ya kwanza Mwl. Julius Nyerere ambaye alisisitiza uwajibikaji katika sekta ya umma kwa manufaa ya umma.BASHE

”Mwalimu Nyerere mwaka 1975 aliwaambia wafanyakazi utii ukizidi unakuwa uoga na siku zote uoga huzaa unafiki na unafiki huzaa kujipendekeza na hivyo huzaa mauti”- Amesema Bashe.

”mwalimu akazidi kuwaambia wafanyakazi kama nyie watumishi wa umma kwa wingi wenu mmeshindwa kupiga kura ya kuwaondoa viongozi dhalimu ni bora mfe”-Amesema Bashe

”Na sisi kama CCM kwa wingi wetu tunashindwa kuishauri serikali kwa ukweli hatuna sababu ya kubaki kuwa madarakan nayasema haya kwa moyo mweupe nikiwa mwanachama wa CCM”-Amesisitiza Bashe.

Aidha Bashe amewasihi mawaziri kuunganisha nguvu ya pamoja katika kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji kwa manufaa ya wananchi kuliko kuachiana kazi hiyo.

HABARI YA HIVI PUNDE: AIBU KUBWA IMEWAKUMBA WABUNGE NA VIGOGO HAWA WANASWA JIJINI TANGA WAKIWA KWA MGANGA MAARUFU WA KIENYEJI WAKITAKA KUMPIGA JUJU RAIS MAGUFULI SHUHUDIA MKASA HUU.....

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’
Mwandishi wetu, Amani
DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’, huenda ndiye mtu anayeongoza kwa kupigwa juju kwa waganga wa kienyeji kuliko mtu yeyote nchini kwa sasa, Amani linakuja na ushuhuda.
Sangoma mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shark Abdullah ‘Kishapu’, akipiga simu kutoka jijini Tanga mwanzoni mwa wiki hii, aliliambia gazeti hili kuwa katika miezi ya hivi karibuni, amekuwa akipata wateja, wakiwemo wafanyabiashara na watumishi wa umma wakimtaka kumpunguza kasi ya utendaji kiongozi huyo, wakisema inawaathiri.
BACK---AMANI“Sikiliza ndugu mwandishi, mimi hapa ni mganga wa kienyeji, nataka nikupe habari. Kuna watu wengi sana wanakuja hapa kwangu kutaka niwakinge na tumbuatumbua ya Magufuli, wengine wanataka nifanye ninavyoweza kumfanya asiweze kutekeleza majukumu yake.
“Nimewapokea wafanyabiashara na hata viongozi wakubwa, wanataka utumbuaji wa majipu usiwapitie, wengine wana madhambi ambayo wanataka yasahaulike ili wasalimike, yaani nakuambia hali ni mbaya,” alisema mganga huyo.
Alipoulizwa kama anawafanyia kama wanavyomtaka afanye, alisema anachokifanya yeye ni kuwapa dawa zinazoweza kuwakinga dhidi ya watu wenye nia mbaya kichawi, lakini si kumroga Rais Magufuli.
Madai ya sangoma huyo yanafanana na Shazoe Mustafa, aliyepiga simu miezi michache iliyopita kutoka Bagamoyo, Pwani ambaye alisema vigogo wengi serikalini, wakiwemo wabunge wamekuwa wakienda kwake kwa ajili ya ‘kumchezea’ Rais Magufuli.
“Kuna wabunge fulani walikuja hapa na kusema nifanye ninavyoweza ili rais awape ulaji. Walisema wanataka uwaziri. Yupo kigogo mmoja wa shirika la umma ambaye alikuwa na hofu ya kutumbuliwa, naye akasema niweke ukungu ili Rais Magufuli asione jina lake. Kila anayekuja kwangu siku hizi ana hofu na kutumbuliwa,” alisema Shazoe.
Hata hivyo, wakati waganga hao  wakipata wateja wengi wanaotaka kinga dhidi ya utumbuaji, waumini wa dini zote wamekuwa hawalali, wakisali na kuswali kuomba ili Mwenyezi Mungu amlinde Rais Magufuli, kwa vile kazi yake ni nzito, yenye maadui wengi.
ASKOFU na Nabii Nicolaus Suguye wa Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM), Matembele ya Pili- Kivule, Dar aliliambia gazeti hili kuwa wamekuwa wakifanya maombi kila mara kwa ajili ya kumuombea ulinzi Rais Magufuli.
“Mara kwa mara tumekuwa na ibada maalum ya kumuombea rais ili pepo wabaya wakae naye mbali. Tunajua vita anayopigana ni kubwa na hatari, binadamu hawezi kumlinda binadamu mwenzake. Sisi tunataka Mungu ndiye afanye kazi hiyo, ndiyo maana tunakesha kwa maombi,” alisema Nabaii Suguye
Daniel Rashid, Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God, Tegeta naye alisema kwa pamoja, waumini wote wamekubaliana kutenga muda maalum wa kumuombea ulinzi kwa malaika ili waifanye kazi ya kuhakikisha kiongozi huyo mkuu wa nchi anakuwa salama.
“Rais Magufuli anafanya kazi kwa manufaa ya wengi, wachache hawapendi na bahati mbaya, hawa wachache ndiyo wenye nguvu, wako serikalini na mitaani, tunajua hatari iliyo mbele yake, ndiyo maana tunamtanguliza Mungu, ni Mungu tu ndiye anaweza kugeuza mioyo ya wahalifu,” alisema.
Licha ya wachungaji hao, pia viongozi wa Kiislamu kutoka misikiti mbalimbali nchini nao wanadaiwa kutenga muda maalum kwa ajili ya kusoma dua ya kumlinda Rais Magufuli, kwani utendaji wake una faida kwa wanyonge wote wa Tanzania.
Juzi, gazeti hili lilimpigia simu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum ili kumuuliza kuhusu hilo kwa upande wake lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

BREAKING NEWS: BUNGE LA JAMUHURI KWA MARA YA KWANZA LIMEWEZA KUFANYA TUKIO LENYE KULETA HAMASA NA KURUDISHA IMANI KUBWA KWA TANZANIA NI BAADA YA WABUNGE VIJANA BUNGENI KUAMUA KUFANYA MAAMUZI HAYA YA AINA YAKE BILA KUJALI ITIKADI ZAO ZA VYAMA SHUHUDIA TUKIO HILI HAPA....

WABUNGE vijana wenye umri usiozidi miaka 40 wameanzisha umoja wao, uitwao Umoja wa Wabunge Vijana Tanzania (TYPG) kwa lengo la kuweka msukumo kwa vijana wote nchini, ndani na nje ya Mwenyekiti wa TYPG ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema), alisema uongozi wa Bunge umepokea vizuri mpango huo na kutoa kibali kwa maandishi cha kubariki uwepo wa umoja huo.

Alisema Spika wa Bunge, Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah waliahidi kwamba uongozi mzima wa bunge utashirikiana na vijana hao, ili wafikie malengo yaliyokusudiwa.

Alisema TYPG inaundwa na wabunge wote wenye umri usiozidi miaka 40, wakiongozwa na Katiba itakayothibitishwa rasmi Juni 2 mwaka huu, siku umoja huo utakapozinduliwa rasmi.

“Tutaweka kando, tofauti za itikadi za kisiasa katika kuendesha shughuli za umoja huu, ndani na nje ya Bunge ili kuweza kufikia azma ya kuungana kwetu,” alisema.

Akizungumzia uongozi wa TYPG, alisema yeye ni Mwenyekiti na Makamu wake ni Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Katimba (CCM), Katibu Mkuu ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (CCM) Naibu wake ni Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema), Mweka Hazina ni mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) na Msaidizi wake ni Hassan Kaunje (CCM), Mbunge wa Lindi Mjini.

BREAKING NEWS: HII NI ZAID YA HATARI KWA WANAFUNZI WA HAWA WOTE WA CHUO KIKUU WATIKIWA KURUDISHA MIKOPO YOTE WALIOPEWA NA HAYA NDIO MAAMUZI MAZITO NA MAGUMU ALIYOFANYA TENA JPM JUU YA SEKTA HII NYETI NA TATA....

Dk. John Magufuli, Rais wa Tanania
RAIS John Magufuli amevunja Kamisheni  ya Tume vya Vyuo Vikuu (TCU) na kuwasimamisha kazi watendaji wakuu wa tume hiyo baada ya kubainika kudahili wanafunzi wasio na sifa na kuwapa mikopo, anaandika Dany Tobason.
Pia serikali imetangaza kufanyika kwa udahili upya Vyuo Vikuu vyote nchi nzima ili kuwaondoa vyuoni wanafunzi wote wasio na sifa sambamba na kutangaza vita kali kwa wanafunzi hewa wanaopata mikopo ya elimu ya juu.
Hayo yamebainishwa leo na Prof. Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipozungumza na waandishi wa habali juu ya kuvunjwa kwa Kamishina ya TCU.
Amesema, kwa idhini aliyopewa na rais anawasimamisha kazi mara moja watendaji hao wa Kamisheni ya Tume ya Vyuo Vikuu.
Prof. Ndalichako amewataja waliosimamishwa kazi kuwa ni Prof. Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU kwa kushindwa kusimamia kazi za TCU akiwa kama mtendaji mkuu wa taasisi hiyo.
Pia, Dk. Savius Maronga, Mkurugenzi wa Udhibiti na Ubora kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kusimamia ubora na ithibati ya Vyuo Vikuu.
Amesema Rose Kiishweko, Mkurugenzi wa Udahili amesimamishwa kwa kushindwa kusimamia udahili wa wanafunzi na kupelekea kudahiliwa wanafunzi wasio na sifa, na mwingine aliyesimamishwa ni Kimboka Istambuli  ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa  Udahili na Nyaraka.
Mbali na hilo Prof. Ndalichako amesema, ili shughuli za TCU ziendelee, Prof. Eliuter Mwageni ameteuliwa kukaimu nafasi ya katibu mtendaji  na kabla ya uteuzi wa kukaimu nahfasi hiyo Prof. Mwageni alikuwa Naibu Makamu Mkuu (Utawala na Fedha) wa Chuo Kikuu cha Ardhi.
 Aidha ameteuliwa Dk. Kokubelwa Mollel ambaye atakaimu nafasi ya ukurugenzi wa udahili na nyaraka na kabla ya uteuzi  wa kukaimu nafasi hiyo Dk. Kokubelwa  alikuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Amesema kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph wanaodahiliwa kutokuwa na sifa.
Waziri amesema, kutokana na hilo serikali imeamua kutoa tamko baada ya ukaguzi kufanyika katika chuo hicho katika kampasi za Arusha na Songea na kubaini kuwepo kwa upungufu mkubwa katika utoaji wa elimu isiyokuwa na kiwango.
Amesema, walibaini kuwepo kwa wanafunzi 489 ambao wapo katika vyuo hivyo ambao hawakidhi viwango na hawana sifa za kusoma Chuo Kikuu.
Amesema kibaya zaidi ni kuwepo kwa wanafunzi ambao ni wa kidato cha nne waliofaulu Daraja la Nne huku wengine wakiwa na pointi 32 lakini wakidahiliwa kusomea shahada ya kwanza .
“Mwanafunzi wa Kidato cha Nne anasoma digrii ya Sayansi, huku mtu huyo akiwa sekondari kasoma mkondo wa biashara lakini kadahiliwa asomee Sayansi na analipiwa mkopo na TCU.
“Si tu hana sifa ya kusoma Chuo Kikuu, hana hata sifa ya kuwa na cheti cha ualimu kwa maana hiyo mtu wa aina hiyo  hafai hata kuwa na cheti cha ualimu hatuwezi kukubali mtu wa jinsi hiyo akasomee digrii,” amesema.
Prof. Ndalichako amesema rais amekuwa akihangaika kutafuta fedha kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu lakini cha kusikitisha kuna wanafunzi waliofaulu vizuri Kidato cha Sita wanakosa mikopo ila wale waliofeli wanapata mikopo hiyo.
“Divisheni four pointi 34 yuko Chuo Kikuu hata ualimu simkubali mtu wa namna hiyo,” amesema.
Amesema, baada ya serikali kufunga chuo hicho wanafunzi hao walihamishiwa vyuo mvingine lakini hata huko walikopelekwa uwezo wao umeonekana kuwa ni mdogo hali iliyolazimu kuwarudisha madarasa ya nyuma.
‘Wanafunzi waliotoka St. Joseph na kupelekwa Chuo Kikuu cha Dodoma uwezo wao umeonekana kuwa ni mdogo, ambapo wanafunzi wa mwaka wa pili na wa kwanza wamerudishwa nyuma muhula moja huku wale wa mwaka wa tatu wamerudishwa nyuma mwaka moja” amesema.
 Amesema, wale wa St. Joseph Tawi la Songea waliopelekwa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA) waliokuwa wakisoma mwaka wa nne wamerudishwa mwaka wa tatu na wametengewa vipindi vya ziada ili kurekebisha upungufu huo, na hata wale waliopelekwa vyuo vingine vya Ruaha, Mkwawa wameonekana kuwa na upungufu pia.
 “Kibaya zaidi hao wanafunzi walikuwa wanapata mikopo, Division four anapata mkopo haki iko wapi, tulipoona jambo hili si sawa, tulichukua hatua tukaieleza bodi ya TCU kusimamisha kazi waliohusika lakini hilo halikufanyika,” amesema.
Kufuatia kuwepo kwa matatizo hayo Prof. Ndalichako ametangaza vita kwa vyuo mbalimbali ambavyo vina watu ambao wanadahili wanafunzi wasio na sifa.
Kuhusu wanafunzi ambao hawakuwa na sifa lakini walikuwa wakisoma chuo kikuu hicho amesema licha ya kuwa wamepoteza muda wao mwingi lakini watalazimika kurejesha mikopo hiyo.
“Wale wote ambao walipata mikopo bila kuwa na sifa watarejesha mikopo hiyo na hakuna njia yoyote ya kuwasaidia bali wanatakiwa kuendelea kuangalia ni jinsi gani ya kujiendeleza,” amesema.

BREAKING NEWS: HII SASA NI ZAIDI YA HATARI MAALIMU SEIFU KUIVURUGA ZANZIBAR AIBUA MAZITO ZAIDI NA YA KUSHANGAZA UMMA BAADA YA TUKIO HILI LA POLISI SHUHUDIA TUKIO HILI HAPA HUKU LISSU AKIFUNGUKA JAMBO ZITO ZAIDI....




Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif
iku moja baada ya Jeshi la Polisi kusema limemwita katibu mkuu wa CUF ijumaa kwa ajili ya kumhoji kuhusu masuala ambayo hayakuwekwa wazi, wanasiasa nchini wamekuja juu wakisema hatua hiyo inaashiria ukandamizaji wa kisiasa, huku chama hicho kikisema kinasubiri tukio hilo ili kitoe msimamo.
Wakati wanasiasa wengi waliozungumza na Mwananchi wakipinga kitendo hicho kwa maelezo kuwa hakitasaidia kutafuta suluhu ya kisiasa Zanzibar, Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa ameshauri wanasiasa kuiga utulivu wa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa licha ya kufanyiwa vitimbi.
Juzi, Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Hamdani Makame alisema, Maalim Seif Sharif Hamad ameitwa kuhojiwa huku Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi akisema kuna mambo mengi ambayo ofisi yake inahitaji kuyafahamu kutoka kwa mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopita.
Lakini wanasiasa wanaona kitendo hicho hakifai.
“Hawa watu wameingia katika njia ya ukandamizaji,” alisema Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki.
“Wameiba kura wakati wa uchaguzi, sasa wanatumia mabavu kuwanyamazisha wote wanaodai haki.”
Msemaji huyo mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alisema Serikali ya CCM inapaswa kujifunza kutokana na makosa na akasisitiza kuwa kumkamata mwanasiasa na kumpeleka Mahakamani si suluhisho, bali ni kuongeza uhasama na ugomvi.
“Maalim Seif aliwahi kuwekwa kizuizini kwa amri ya Mwalimu Nyerere (Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza) mwaka 1987 hadi 1991, lakini hiyo haikusaidia chochote. Maalim aliwahi kufunguliwa kesi ya uhaini lakini haikusaidia chochote,” alisema Lissu.
“Yaani huo uamuzi wa polisi kumhoji Maalim unaonyesha kuwa hawa watu hawajifunzi kutokana na historia ya nchi yetu.”
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alikosoa njia ambayo polisi wametumia.
Alisema badala ya kumuita kituo cha polisi, walitakiwa kuomba kukutana naye na kumfuata popote alipo na kuomba maelezo yake.
Alisema kitendo cha kumwita polisi na hali ya sasa ya Zanzibar ni kuchochea uhasama kati ya wananchi na Serikali.
Mbatia, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alimshauri Rais John Magufuli, ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, awatake polisi kusitisha mpango huo.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya alisema: “Tunaisubiri siku ya Ijumaa kwa hamu. Tutajua hatua ya kuchukua kama chama baada ya kuona hatua ambazo Maalim atachukuliwa.”
Kambaya alitaja makada wa CUF ambao alidai wamekamatwa na kuhojiwa na polisi kuwa ni Nassor Ahmed Mazrui, Mansoor Yussuf Himid na mwanamkakati wa Maalim Seif katika chaguzi zilizopita, Mohamed Sultan Mugheiry, maarufu kwa jina la Eddy Riyami.
Ismail Jusa Ladhu alisema sababu kubwa ni Uchaguzi Mkuu pamoja na ule uliofutwa, kauli ambayo iliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho-Bara, Magdalena Sakaya.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Hamad Masoud Hamad alisema hatua hiyo ni njia mbadala ya kuwanyamazisha Wazanzibari ambao alidai kuwa wengi waliamua kumpa ridhaa Maalim Seif kuiongoza Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu ambao matokeo yake yalifutwa.
Alisema katibu huyo mkuu wa CUF ni kiongozi aliyekubalika kwenye nyoyo za Wazanzibari wengi, hivyo hatua ya kujenga hofu na mazingira ya kumdhalilisha hayatawarudisha nyuma.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Salim Abdalla Bimani alisema huu si wakati tena wa siasa za kutishana kwa kuitiana polisi kwa kuwa Wazanzibari wameshakuwa wanaelewa kila hatua na njia bora za kudai haki.
Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar, Habibu Ismail Rashid alisema: “Nahisi hii ni njia ya kutaka kumdhalilisha Maalim Seif ili atoke mioyoni kwa watu, lakini nawaambia hilo wasahau. Maalim Seif anapendwa bwana!”
Viongozi wa upinzani, hasa kutoka CUF wamekuwa wakihojiwa na Jeshi la Polisi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20.
Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais. Alifuta matokeo hayo wakati ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31, huku mengine tisa yaliyosalia yakiwa yameshahakikiwa.
Alisema sababu za kufuta matokeo hayo ni kukiukwa kwa sheria na kanuni za uchaguzi, lakini CUF ilipinga ikisema alichukua uamuzi huo peke yake na kususia kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio.

HABARI YA HIVI PUNDE: KUTOKA BUNGENI BUNGE LAWAKA MOTO HIVI PUNDE BAADA YA KITIMTIMU CHA WABUNGE MAJANGILI KUTAKIWA KUPIGWA RISASI HUKU MAGIGE NA MAGHEMBE WAKINUKISHA BUNGENI NA KUENDELEA KUZUA HOFU KUBWA KWA WABUNGE HAWA MAJANGILI SHUHUDIA TUKIO HILI HAPA.....

MBUNGE wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM) amesema Bunge linapaswa kufahamu ni mbunge gani ambaye anajihusisha na ujangili, kwani hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria.

Magige, ambaye amependekeza sheria ibadilishwe majangili ama wapigwe risasi au wafungwe jela maisha, ni miongoni mwa wabunge ambao walivalia njuga suala la ujangili jana wakati wakichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.MAGHEMBEKwa upande wake, serikali kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17, alisema majangili nguli wanane wenye mitandao ya kimataifa ni miongoni mwa wahalifu 53 waliohukumiwa baada ya kukutwa na hatia.

Wabunge majangili? Akichangia, mbunge Magige alisema inasemekana baadhi ya wabunge wanajihusisha na ujangili hivyo akashauri ni vyema wakafahamika. “Inasemekana baadhi ya wabunge wanajihusisha na ujangili. Huyo jangili ni nani? Munde Tambwe, Catherine Magige au Ally Keissy,” alihoji mbunge huyo wa Viti Maalumu kutoka Mkoa wa Arusha. “Hakuna aliye juu ya sheria, tunaambiwa majangili tunao humu ndani, tunataka tuwafahamu, tusinyooshee vidole wengine,” aliongeza Magige.

Alisema ujangili umekithiri nchini na tembo wanatoweka. Alipendekeza sheria ibadilishwe majangili ama wapigwe risasi au wafungwe jela maisha. Majangili nguli watajwa Profesa Maghembe alisema katika mwaka 2015/16, doria zilifanyika ndani na nje ya Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu kwa siku-doria 109,474 na ziliwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 1,176 na kesi 654 zilifunguliwa.

BREAKING NEWS: HAYA NDIO MAAMUZI MAGUMU NA YALIYOFANYWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM VIGOGO 29 NDANI YA CCM KUVULIWA UWANACHAMA BAADA YA KUBAINIKA NA USALITI HUU MKUBWA NDANI YA CHAMA CCM SASA KUJISHAFISHA KWA STAILI HII SHUHUDIA TUKIO HILI....

WANACHAMA 29 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamevuliwa uanachama na wengine sita kushushwa vyeo mkoani Shinyanga, kutokana na kile kilichoelezwa ni kukisaliti wakati wa uchaguzi mkuu. Miongoni mwa waliovuliwa uongozi ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Shinyanga Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe alisema uamuzi huo umetokana na kikao cha Halmashauri Kuu. Wengine waliovuliwa madaraka na vyeo vyao katika mabano ni Edward Lubinza (Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya) na Ng’honge Nkwabi (Kamanda wa UVCCM ) ambao wote ni wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Pia aliwataja wengine na vyeo vyao kwenye mabano ni Charles Nkwabi (Katibu Kata ya Kisuke) kata ya Ngogwa, Wilfred Sazia (Mwenyekiti Kata Ngogwa), Samwel Gachu ambaye ni Katibu Mwenezi kata ya Isaka. Viongozi wengine waliovuliwa nyadhifa ni Peter Kigingi (Mwenyekiti Kata ya Bukomela) na Japhet Mabula ambaye ni Katibu Kata ya Mjini Kahama.

Kusilawe alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM Toleo la mwaka 2012 Ibara ya 93, Kifungu kidogo cha 14 kinatoa mamlaka kwa Halmashauri Kuu ya Mkoa, kumchukulia hatua mwanachama yeyote atakayedhihirika kukosa sifa ya chama hicho.

HABARI YA HIVI PUNDE: HII NI KUTOKA BUNGENI BUNGE LAZIDI KUSHIKA KASI MAJI MAREFU AWALIPUA WABUNGE HAWA NA KASHFA NZITO YA NHC NA KUZUA TAHARUKI YA AINA YAKE.....

MBUNGE wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (CCM), maarufu kwa jina la ‘Maji Marefu’ amewalipua wabunge waliokosa ubunge katika kipindi hiki na vilivyopita kwa kuhodhi nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mjini hapa na kupangisha watu wengine kinyume cha utaratibu wa shirika Alisema hali hiyo imefanya wabunge wapya, ambao ni asilimia 70 ya wabunge wote kwa sasa, kukaa nyumba za kulala wageni wakati zipo nyumba hizo kwa wabunge kulingana na mkataba na NHC.

Mbunge alisema wapo watu wamepangishwa na wabunge hao wa zamani, ambao wamegeuza nyumba hizo kama kitega uchumi kinyume na taratibu. Ngonyani alisema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Alimuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kufuatilia suala hilo na shirika kwa ujumla, aondoe wapangaji hao waliowapangishia wengine kinyume cha utaratibu na kuwapatia nyumba wabunge wapya ambao hawana nyumba za kuishi.

Alisema wabunge hao waliokosa nafasi ya kurudi jimboni miaka tofauti, mkataba wao wa kupangishwa nyumba hizo umekwisha, kwani ukishakosa ubunge hauna dhamana tena mpaka utakaporudi.

“ Kuna wapangaji wengi ambao ni wabunge waliokosa nafasi hiyo ambao wamepangishwa na shirika na badala yake hadi leo wamezishikilia nyumba hizo hawataki kuziachia, ”alisema Ngonyani.

BREAKING NEWS: HII NI TAARIFA MUHIMU MAKOMANDO JWTZ KUTUMIA DK 180 KUFANYA TUKIO LA AINA NA LA KUSHANGAZA UMMA NI PALE WALIPOFANYA UVAMIZIKATIKA MAPANGO YA AMBONI NA KUIBUA KUNDI HILI KUBWA LA MAGAIDI LILOFANYA TUKIO LA MSIKITINI HIVI JUZI SHUHUDIA MTIFUANO HUU....





IMG_20160524_052830

BREAKING NEWS: NI HABARI NJEMA SANA KWA MISS TANZANIA MWAKA 2006 MADAAM WEMA SEPETU KUINGIA KATIKA HISTORI HII KUBWA KWA TANZANIA NA AFRIKA NZIMA NI B YA KUZINDUA MOBILE APP...


Tafiti za hivi karibuni zinaonesha zaidi ya nusu ya matajiri wajasiriamali duniani ni Wachina ambapo wataalamu wanasema hii inatoka na muasisi wa nchi hiyo Mao kutamka kuwa wanawake wanamiliki nusu ya mbingu hivyo kuanzia hapo ndio ulikuwa mwanzo wa wanawake wachina kuamka na kuanza kujituma.

Matajiri wakubwa wanawake wanaotokea china ni Zhang Yin, Wu Yajun na Chen Lihua; wengine ambao sio Wachina ni Oprah Winfrey ambaye anaaminika kumiliki utajiri mkubwa kutokana na jitihada anazozifanya.

Hali kadhalika kwa upande wa Tanzania kumekuwa na mwamko kwa wanawake wanaojitambua kuamua kufanya ujasiriamali kwa kubuni biashara binafsi ambazo huwaingizia kipato mfano Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania Flaviana Matata aliyezindua hivi karibuni rangi za kucha ikiwa ni moja ya mbinu za kujikwamua.

Sasa baada ya mlimbwende Wema Sepetu kuzindua ‘lipstick’ ya Kiss, mapema jana aliamua kuongeza wigo wa biashara kwa kuzindua ‘app’ yake ambayo itakuwa inahusisha stories zake binafsi, zenye ukweli na uhakika na mashabiki zake wataweza kupata video clips, audio na picture zinazomhusu mrembo huyo.

Wema amevunja rekodi kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania na Afrika kumiliki ‘Mobile App’, kama ambavyo Kapteni Hilda Wendy Ringo alivyovunja rekodi kuwa mwanake wa kwanza kurusha ndege Tanzania.  Mobile Application ya Wema sepetu itapatikana kwa watumiaji wa ‘smart phone’ simu za kawaida.

HABARI YA HIVI PUNDE: HII NDIO CCM YA JPM BANA HAYA SASA NDIO MAAUMAZI YALIOACHA GUMZO LA AINA YAKE BAAADA YA MSEMAJI WA CCM OLE SENDEKA KUTOA TAARIFA HII JUU YA MSIMAMO WA CCM BAADA YA TUKIO LA KITWANGA SASA RASMI ATAKAE CHUKUA NAFASI YAKE KUJULIKANA MSIKILZE HAPA MSEMAJI HUYU MACHACHARI...



CCM imesema kitendo cha Rais John Magufuli kumvua uwaziri Charles Kitwanga kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa, kimedhihirisha kuwa bado kuna baadhi ya watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma, lakini hakitachukua hatua kwa kuwa ameshaadhibiwa.

Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka jana  alisema kitendo cha Kitwanga kuingia bungeni akiwa amelewa kimewapa fundisho na sasa wanajua kuwa kuna baadhi ya watumishi waliopewa dhamana na chama hicho, lakini wanakiuka miiko ya maadili ya utumishi wa umma, jambo ambalo ni kinyume na taratibu zao.

Sendeka alisema licha ya kwamba Rais Magufuli amechukua hatua juu ya hilo na kutoa adhabu, CCM itaendelea kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya wanasiasa waliopewa dhamana na chama hicho.

“Hatutasita kuchukua hatua endapo tutabaini kuna kada anayekiuka maadili ya viongozi wa umma,” alisema Sendeka.

Alisema CCM inampongeza Rais Magufuli kwa uamuzi aliochukua dhidi ya Kitwanga kwa kuwa hatua hiyo imedhihirisha kauli aliyowahi kusema kwamba hataangalia mtu usoni wala kujali kabila au dini, ikiwa mtu huyo atakiuka miiko ya uongozi.

Kuhusu CCM kumuadhibu Kitwanga, Sendeka alisema adhabu aliyopewa na Rais inatosha. “Hukumu haitolewi mara mbili,” alisema Sendeka.

Kitwanga ambaye anatajwa kwenye sakata la utekelezaji mbovu wa mkataba wa kufunga vifaa vya kuchukua alama za vidole baina ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises, alivuliwa ukuu wa wizara hiyo nyeti baada ya kutinga ndani ya ukumbi wa Bunge Ijumaa asubuhi na kujibu maswali akiwa amelewa.

Hadi jana jioni, Rais Magufuli alikuwa bado hajajaza nafasi hiyo nyeti huku wananchi wakibashiri jina la mrithi wa Kitwanga kwa kuangalia jinsi marais waliopita walivyokuwa wakijaza nafasi kama wa kumpandisha naibu waziri wa wizara hiyo au nyingine, kumteua mtu anayemfahamu, kubadilisha mawaziri na kumrejesha aliyewahi kuwa waziri ama kuteua kutoka kwenye kanda anayotoka aliyetimuliwa.

Mara nyingi katika uteuzi wa mawaziri, viongozi wakuu wa nchi wamekuwa na utaratibu wa kuwapandisha baadhi ya manaibu kuwa mawaziri, kuwapa uwaziri wabunge ambao amewateua au kuteua waziri kutoka katika mkoa ambao anatokea waziri aliyeondolewa.

Mara zote saba ambazo Rais mstaafu Jakaya Kikwete alifanya mabadiliko ya baraza la mawaziri alifuata utaratibu huo.

Alipomuondoa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye ni mbunge kutoka mkoa Kagera alimteua mbunge mwingine kutoka mkoa huo, Charles Mwijage kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini.Kwa sasa Mwijage ni Waziri wa Viwanda na Biashara.

Utaratibu huo unaweza kunufaisha wabunge sita wa majimbo yaliyopo mkoa wa Mwanza ambao ni Chalres Tizeba (Buchosa), Mansoor Hirani (Kwimba), Kiswaga Boniventura (Magu), Stanslaus Mabula (Nyamagana), William Ngeleja (Sengerema) na Richard Ndassa (Sumve).

Mbali na Kitwanga ambaye aliteuliwa kuwa waziri kutoka mkoa huo, Rais pia alimteua mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Iwapo Rais atatumia utaratibu wa kupandisha naibu waziri kuwa waziri, neema huenda ikamuangukia mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandishi Hamad Masauni au naibu mawaziri kutoka wizara nyingine. Katiba pia inampa Rais fursa ya kuteua wabunge 10 na tayari ameshatumia nafasi sita.

BREAKING NEWS: BUNGE SASA LAZIDI KUPAMBA MOTO NI MSHIKESHIKE ULEULE SPIKA WABUNGE KUWAWEKA BAYANA WABUNGE WOTE WAVUTAO UNGA PAMOJA NA BANGI ADAI KIKAO CHA MCHANA NDIO MAJANGA MSHUHUDIE HAPA SPIKA AKIFICHUA WABUNGE HAWA.....

IMG_20160523_045912

BREAKING NEWS: KATIKA HALI ISIYOKUWA IKITEGEMEWA MKE WA SAJENTI ALLY KINYOGOLI KAMANDA ALIEUWAWA HAPO JUZI NAEATIWA MBARONI MTOTO WA MAREHEMU ASIMULIA MAZITO....

Watu 15 akiwamo mke wa marehemu, Sajenti Ally Salum Kinyogoli wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na tukio la kuuawa kwa askari huyo wa kikosi cha usalama barabarani usiku wa kuamkia jana.

Kinyogoli aliyezikwa jana saa 10 jioni kwenye Makaburi ya Mzambarauni, Kitunda, Dar es Salaam alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na kutoa taarifa kuhusu hali ya usalama barabarani katika vyombo vya habari.

Kinyogoli aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake, Chatembo Kata ya Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani mbele ya mtoto wake, mwenye umri wa miaka kumi na moja.

Akizungumzia kukamatwa kwa mjane huyo, Kamanda wa Kipolisi Temeke, Gilles Muloto alisema:
“Sidhani kama mnaweza kuzungumza naye kwa sababu hao waliomshikilia ni polisi na wanakwenda naye kituoni. Hata hivyo, mimi siyo msemaji wa hili anayeweza kulizungumzia ni Kamanda wa Mkoa wa Pwani.”

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi ambaye hakuwapo msibani alipopigiwa simu ilipokewa na mpambe wake ambaye alisema: “Mkuu leo amebanwa na vikao vingi kuna Mwenge mkoani kwake na hili tukio la kusikitisha.”

Mgogoro wa kifamilia
Mama mlezi wa marehemu, Coletha Ndima alisema mara ya mwisho kuonana na Kinyogoli ni juzi wakati marehemu alipopeleka baadhi ya samani zake kwa kile alichodai mke wake mkubwa alikuwa akiziuza.

“Hatujui kama kuna mgogoro lakini Kinyogoli aliwahi kutuambia kuwa anataka kuoa mke wa pili, sijui alishaoa, kwa sababu alisema atakuja kumtambulisha mchumba lakini hakufanya hivyo,” alisema.

Ndima alisema marehemu aliwahi kumwambia kuwa ana mgogoro na mkewe mkubwa lakini hajui ni wa nini.

Mmoja wa polisi ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema polisi wanamshikilia mama huyo kwa kuwa yeye ndiye aliyemuita Kinyogoli aende nyumbani kwake na mauti kumfika.

“Marehemu alitengana na mke wake mkubwa, lakini siku moja kabla ya kifo, mama huyo alimuita akimwambia watoto wamemkumbuka, usiku huohuo, ndipo walipomuua,” alisema.
Mtoto asimulia mauaji yalivyotokea

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Ebenezer iliyopo Mwandege alieleza kuwa watu wawili walifika nyumbani hapo na kumtaka amuite baba yake.

“Nilipoingia ndani kumuita baba, nilimkuta anatandika kitanda, baba akaniambia waambie nakuja, wakati natoka, baba naye alikuwa nyuma yangu, lakini niliwakuta wale watu safari hii wamevaa ninja (mask) lakini kabla ya hapo walikuwa hawajavaa,” alisema.

Alisema watu wale walianza kumkaripia baba yake wakimtaka awape funguo ya gari lakini alikuwa akibishana nao na kisha kuanza kupambana nao lakini walimpiga bastola ya kichwani na mbavuni.

“Wakati baba anapambana nao alikuwa anawauliza nimefanya nini, lakini hawakumjibu, alianza kupiga kelele, wanangu nakufa, wanangu nakufa,” alisimulia kuongeza:

“Ujue baba alishawaweza wale, lakini walivyoona anawashinda nguvu waliamua kumpiga bastola.”
Baba wa marehemu, Salum Kinyogoli aliwataka polisi kufuatilia suala hilo ili wahalifu hao wapatikane.

Dada wa marehemu, Zainab Kinyogoli aliyeonekana kuchanganyikiwa kutokana na msiba huo alikuwa akilia mfululizo huku akisema: “Ally aje nimbebe, nimemuachia ziwa, nimembeba.”
Maelezo ya polisi

Awali, Kamanda Mushongi aliwaambia waandishi wa habari mjini Kibaha kwamba wauaji hao walifika nyumbani kwa askari huyo wakitumia pikipiki aina ya Boxer na waliingia ndani kwa kuruka uzio.

Hata hivyo, wauaji hao walipofika kwenye gari hilo hawakufanya lolote bali walitelekeza ufunguo huo na kutokomea.

“Naweza kusema ni tukio la kushtukiza kwa kweli kwa sababu ilikua ni muda mfupi tu toka askari aliporudi nyumbani kwake akitokea kazini na hawa wauaji hawakuchukua kitu maana hata ufunguo wa gari waliouchukua pale nyumbani walitoka nao nje na kuuacha,” alisema Mushongi.

KIMENUKA TENA UKAWA MUDA SI YREFU KIGOGO HUYU MZITO WA CCM ATOA TAMKO LA KUTAKA ALIYEKUWA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CUF HUKO Z'BAR "MAALIM SEIF" AKAMATWE KWA KAULI HIZI ALIZOZITOA HADHARANI

Kigogo wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake aliyoihusisha na kosa la uhaini.

Sukwa aliitaja kauli ya Maalim Seif aliyoitoa alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba kuwa Dk. Ali Mohamed Shein hatamaliza kipindi chake cha urais mwaka 2020 na kwamba ni dikteta.

Sukwa amesema kuwa kauli hiyo ya Maalim Seif haipaswi kupuuzwa hata kidogo kwakuwa kauli kama hizo ni zaidi ya sumu.

“Sivilazimishi vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri tu visipuuze ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko matendo yake,” Sukwa aliliambia gazeti la Raia Tanzania.

Maalim Seif amekuwa akifanya mikutano kuwataka wananchi kumuunga mkono kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Shein, akieleza kuwa uchaguzi wa marudio haukuwa wa haki.

CHANZO: UDAKUSPECIALLY
Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top