Loading...

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MZITO TBC,NSSF NA RAHCO: HAWA NDIO WALIOPEWA UKURUGENZI WA MASHIRIKA HAYO

Profesa Godius Kahyarara, Mkurugenzi mpya wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Profesa Godius Kahyarara, Mkurugenzi mpya wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Pamoja na hivyo Rais Magufuli amemteua Dk. Ayub Rioba kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) ambapo Dk. Mussa Mgwatu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO).
Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam imearifu kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.
Prof. Kahyarara amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Ramadhan Dau ambaye kwa sasa anasubiri kupangiwa uwakilishi wa nchi (ubalozi).
Prof. Kahyarara ni mchumi mbobezi kitaaluma na ndiye Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Jamii (COSS) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Dk. Rioba Mkurugenzi mpya wa TBC alikuwa Mkuu wa Shule Kuu ya Habari na Mawasiliano kwa Umma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amefikisha umri wa kustaafu.
Dk. Mgwatu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa kutokana na utendaji usioridhisha.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, imearifu kuwa uteuzi huo unaanza kazi mara moja baada ya kutangazwa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top