VIGOGO wawili raia wa Kichina, Huang Gin na Yu Fujie waliokamatwa mwaka 2013 wakituhumiwa kukutwa na meno ya tembo wamehukumiwa kwendea jela miaka 30 au kulipa shilingi Bilioni 54 kila mmoja.
Raia hao wamehukumiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam chini ya Hakimu Mkazi, Cyprian Mkeha ambapo kesi hiyo ilichukua muda wa zaidi ya saa 5 kusomwa huku upande wa serikali kupitia kwa Wakili wa Serikali ukiongozwa na Faraja Nchimbi ambaye alikuwa na mawakili wengine ambao ni Paul Kadushi,Wankyo Simon pamoja na Salim Msemo ambapo kwa upande wa washitakiwa waliwakilishwa na Wakili Nehemiah Nkoko ambaye alijaribu kutoa hoja zake ikiwemo kuiomba mahakama iwapunguzie adhabu.
Watuhumiwa wote walisomewa mashtaka matatu ambayo ni kwanza, kukamatwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo, shitaka la pili, kutumia pesa walizokutwa nazo katika upekuzi kuwashawishi maofisa wa serikali ili wawaachie na shitaka la tatu, kukutwa na ganda la risasi katika nyumba waliyokuwa wakiishi ambapo shitaka hilo la tatu lilitupiwa mbali na kubaki mawili yaliyowatia hatiani.
Akisoma vifungu vya sheria, Hakimu Mkeha alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa Novemba 2013 katika nyumba waliyokuwa wamepanga iliyopo Mikocheni jijini Dar, wakiwa na vipande vya meno ya tembo 728 ambapo ni sawa na tembo waliouawa 226 na kusema kuwa waliisababishia serikali kupoteza fedha nyingi na kuingizwa katika kesi ya uhujumu uchumi. Pia mahakama iliamuru magari yao matatu waliyokutwa nayo kutaifishwa.
Mshitakiwa wa pili,Yu Fujie (kushoto) na Huang Gin wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakiingizwa katika chumba cha mahakama na askari magereza.
Wakijuta baada ya kuhukumiwa.
Post a Comment