Taarifa za usajili wa Yanga zimekuja wakati watani zao, Simba wakimkabidhi rungu kocha wao, Jackson Mayanja kuanza mapema mikakati.
YANGA imetanguliza ‘kachero’ Misri wa kuipeleleza Al Ahly huku usajili wao mpya ukivuja mapema ikidaiwa wanasaka vijana wa kazi wasiopungua watatu.
Taarifa za usajili wa Yanga zimekuja wakati watani zao, Simba wakimkabidhi rungu kocha wao, Jackson Mayanja kuanza mapema mikakati.
Hitaji la kikosi hicho chini ya Kocha Hans Pluijm ni kiungo mkabaji wa chini ambaye atakuwa na ubora mkubwa ili kuwapunguzia majukumu mabeki wa kati, kwa sasa anakosekana mtu wa hitaji la benchi la ufundi.
Pluijm anaonekana kukosa mtu sahihi wa kuhimili kasi anayotaka, mkongwe Mbuyu Twite aliyekuwa akicheza nafasi hiyo anaonekana kupungua makali kiasi cha kuhamisha akili ya makocha wake kwa Patrick Ngonyani na hata Salum Telela aliyecheza dhidi ya Al Ahly jijini Dar es Salam na mechi kuisha kwa sare ya bao 1-1. Inaelezwa kuwa anasakwa beki wa kati baada ya kukosekana nahodha wao Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na hivyo kuamsha akili mpya Yanga ambao pia wanatafuta mtu sahihi wa nafasi hiyo baada ya kuona Cannavaro hajaweza kurudi katika ubora unaohitajika anapocheza na Kelvin Yondani anayeonekana kuibeba safu hiyo na Vicent Bossou kuanza kufanya makosa mengi kwa kuruhusu mabao katika mechi za karibuni.
Jicho limeelekezwa zaidi kwa Salim Mbonde wa Mtibwa ambaye msimu huu nusura avae uzi wa Yanga.
Yanga bado inataka kiungo wa pembeni mwenye makali kumzidi Isouffou Boubacar ambaye bado hajaweza kuhimili kasi yao ingawa ameanza kupewa mechi ili athibitishe ubora wake tangu apone.
Changamoto ya nafasi hizo Yanga inatokana na kukamilika idadi ya wachezaji wa kigeni na akili iliyopo ni kukata mchezaji wa kigeni atakayeshindwa kukidhi kifungu cha mkataba cha kucheza chini ya kiwango cha 10% ya mechi za Yanga kama walivyokatwa Jerry Tegete, Hussein Javu na Rajab Zahir usajili uliopita.
Yatuma kachero Misri
Yanga haijakata tamaa kuelekea mechi ya marudiano na Ahly na tayari imetuma mtu aliyeondoka jana Jumatano kuwapeleleza Ahly.
Ingawa Yanga imefanya siri kubwa, Mwanaspoti linafahamu mtu wa kwanza ametangulia Misri kufanya kazi tatu. Kiongozi huyo atatakiwa kutafuta hoteli ya timu kufikia lakini pia ametakiwa kusaka sehemu sahihi ambayo Ahly wanapenyezea fitina zao baada ya Pluijm kudokeza kwamba viongozi wakijiongeza kidogo kutumia gharama kuelekea mechi hiyo wanaweza kushangaza wengi. Bosi huyo ambaye pia alitangulizwa Rwanda na kuandaa mazingira bora ambayo Yanga iliyatumia kuvuna ushindi wa mabao 2-1, ametakiwa kuhakikisha anajua mipango ya kikosi chao kikiwa Alexandria mchezo huo utakapochezwa baada ya mechi kuondolewa jijini Cairo
Post a Comment