Loading...

HABARI YA KUSIKITISHA: MASANII MDOGO NA MAARUFU TZ "DOGO JANJA" APATA PIGO ZITO NA KUMFANYA AJUTIE UMAARUFU WAKE

Rapa wa Tip Top Connection, Dogo Janja amesema ana mpango wa kurudi shule kutokana na muziki wake pamoja na maisha kuhitaji elimu yakutosha.

Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Dogo Janja amesema kuna wakati anajuta kabisa kutomaliza shule.

“Kusema kweli najuta kutomaliza shule,” alisema Dogo Janja. “Msanii lazima uwe pande mbili, huwezi kuwa msanii wakati wote, kuna wakati utahitaji kufanya mambo mengine,”

Dogo Janja amesema muziki ndio kitu ambacho kilimsabisha ashindwe kuzingatia masomo.

“Nilikuwa nikifungua radio au TV kote nazungumziwa, stress zikawa zinanichanganya nikawa sisomi, bila stress ningesoma na ningefaulu. Nampango wa kurudi shule za private, kwa sababu elimu ni kila kitu,” alisema Dogo Janja.

Pia Janjaro amewataka vijana walio mashuleni kuzingatia masomo yao kwa elimu ndio kila kitu katika maisha.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top