Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz Ferooz alidai kuwa yeye anaona ni bora mtu apate Ukimwi kwani itawezekana mtu huyo kuishi kwa matumaini, huku akiendelea kufanya mambo yake ya msingi katika jamii na kudai tofauti na mtumiaji wa dawa za kulevya kwani hataweza kufanya jambo lolote la maendeleo.
“Madawa ya kulevya ni zaidi ya kupata HIV, ni mara kumi upate Ukimwi kuliko ukiwa unatumia madawa ya kulevya, sababu Ukimwi unaweza kuishi kwa matumaini na ukatumia madawa za ARVs ukaishi miaka mingi ukadumu,lakini madawa ya kulevya utaadhirika na hautafanya kitu chochote katika maisha yaani utakuwa ‘nothing’ (bure) katika maisha, kwa hiyo ni tatizo baya zaidi hivyo madawa ya kulevya si ya kuyasogelea kabisa,” alisema Ferooz.
Mbali na hilo Ferooz alieleza kuwa wasanii wengi wanajikuta wanaingi kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na msongo wa mawazo kwa kazi zao kutochezwa kwenye vyombo vya habari na kazi hizo kutopokelewa vyema na mashabiki jambo ambalo linawapelekea kuwaza sana hivyo wengine wanaona njia ya kupunguza mawazo hayo ni kunywa viroba kama si kwenda kutumia dawa za kulevya
Post a Comment