Loading...
Home
»
NEWS
»
BREAKING NEWS: HILI NI TUKIO LA HESHIMA NA KUIGWA JUU YA ALICHOKIFANYA MBUNGE WA UKONGA MWITA WAITARA LEO BILA KUJALI ITIKADI ZA KICHANA NI NDANI YA JIMBO LAKE LEO HII....
Ndoto za Watanzania wengi ni kuona viongozi waliowachagua wanawatumikia kwa nguvu zote kwa kuwaletea maendeleo yatakayo wanufaisha bila kujali itikadi za aina yeyote, kwani kuwepo kwa maendeleo katika jimbo husika ni faida ya wananchi wote.
Hivyo kwa kuzingatia hayo mfuko wa jimbo la Ukonga chini ya mwenyekiti wake ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo Mwita Waitara umetoa kiasi cha shilingi milioni 17 kwa ajili miradi ya maendeleo ya Jimbo hilo jambo ambalo ni faraja kwa wanachi wa maeneo hayo waliokuwa wanasumbuliwa na kero mbalimbali.
Moja ya kero zilizokuwa kikwazo cha muda mrefu kwa wakazi wa Kata ya kipunguni ni kutokuwepo kwa Kivuko katika shule za Kilimani na Kipunguni ambapo mfuko wa Jimbo umetenga kiasi cha milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko ili wanachi wanafunzi waondokane na adha waliyokuwa wakikumbana nayo na kulazimika kuingia kwenye maji ambayo ni hatari kwa Afya.
Akizungumza na mtembezi.com Diwani wa Kata ya Kipunguni Mohamed Msofe amesema wamefarijika sana baada ya pesa hizo kuingizwa kwenye mfuko jimbo hivyo anaimani ujenzi huo utaanzaa haraka iwezekavyo, huku akiwataka wadau mbalimbali kuchangia miradi ya maendeleo ya kata hiyo kwani serikali pekee haitoweza bila ya kuwepo kwa nguvu za wadau.
Filed Under:
NEWS
Friday, 27 May 2016
Post a Comment