Loading...

BREAKING NEWS NI ZAIDI YA AIBU NI LAANA CHAFU ALIOYOFANYA MSHAURI WA RAIS SHEIN KUTWA AKILA ARODA BINTI MDOGO WA MIAKA 20 HILI NI TUKIO LA PILI TENA ZANZIBAR....

Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar (katikati) akipokea ripoti kutoka kwa Dadi Faki Dadi aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
SERIKALI ya Dk. Ali Mohammed Shein imezama kwenye aibu, ni baada ya mshauri wake Dadi Faki Dadi kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na mwanaye, anaandika Pendo Omary.
Faki alikuwa Mkuu Mkoa wa Kaskazini Pemba lakini baada ya kukosa nafasi hiyo katika ngwe ya pili ya Dk. Shein, aliteuliwa kushika nafasi hiyo ya ushahuri kwa rais hususan masuala ya yanayohusu Pemba.
Mshauri huyo amekamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na mtoto wake wa kambo (mtoto wa mkewe) mwenye umri wa miaka 21.
Mwanasiasa huyo maarufu visiwani humo alikamatwa mbele ya mkewe na baadhi ya wanafamilia juzi katika nyumba ya wageni ya Executive, jirani na Makao Makuu ya Uhamiaji Zanzibar, eneo la Kilimani mjini Unguja na kupelekwa katika kituo cha Polisi Mwembemadema.
Mkadam Khamis, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi amethibitisha kushikiliwa kwa Dadi na polisi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.
“Tunaendelea kufanya uchunguzi. Iwapo tutabaini ametenda kosa tutampeleka katika vyombo vya sheria,” amesema Khamis.
Aidha, picha za video ambazo zinaendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii zinamuonesha Dadi akishambuliwa kwa maneno makali kutoka kwa mkewe na watu waliomkamata.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top