Loading...
Home
»
MATUKIO
»
NEWS
»
SIASA
»
BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI SASA HASHIKIKI TENA HII MOJA YA TUKIO LA KIHISTORIA KATIKA UTAWALA WAKE MPAKA SASA AMUA WAZIWAZI KUPINGANA NA UKWELI WA JAMBO HILI NA KUAMUA HAYA....
anayepingana na ukweli kwamba ‘Wazee ni hazina ya Taifa la Tanzania’ lakini acha ukweli uzungumzwe, kwani ‘kubebana’ na‘kuleana’ kumetufikisha hapa tulipo.
Tabia iliyojengwa na wazee ya kufanya kazi kwa mazoea huku waking’ang’ania madaraka kunalifanya taifa kupiga ‘mark time’ badala ya kusonga mbele; tafiti zinaonesha asilimia kubwa ya vijana wasomi wapo mitaani na hawana ajira kutokana na nafasi hizo kukaliwa na wazee, tena ambao hawana elimu sawa na vijana wasomi ambao wanasota mitaani.
Jambo hili linamfanya Rais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuamua kufanya kazi na vijana katika serikali yake kwani amegundua licha ya vijana wachapakazi kutopendwa na baadhi ya watu, ni wachapakazi na watamsaidia kulipeleka taifa katika maendeleo anayoyatamani, kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawapendi rushwa.
“Nimegundua vijana wengi hawapendi rushwa, hivyo nitaongeza vijana kila nikiteua kwa kuwa niliowaweka naona matunda ya kazi zao, najua watu wanawachukia sana ila nitawaongeza. Palipo na vijana nimeona mambo yanaenda na kuna mabadiliko. Wazee ndio tumelifikisha taifa hili hapa, hakuna asiyejua kuwa Tanzania ilichakaa kila mahala”.
Ni wazi hivi sasa wazee wamekalia kuti kavu katika Serikali ya Awamu ya Tano kwani Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amefuata nyayo za Rais Magufuli katika ‘operesheni fukuza wazee’ baada ya kutamka wazi kwamba wakati umefika kwa wazee wanaofanya kazi katika Kampuni ya Simu ya TTCL kuwaachia Vijana kwa sababu wazee wamekua watu wa kuzungumza zaidi kuliko vitendo kwani Sekta ya Mawasiliano hivi sasa ina ushindani mkubwa.
Post a Comment