Loading...

Dudu Baya Aongea haya Baada ya Chidi Benz Kudaiwa Kutoroka ‘Sober House’

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Dudu Baya amesema kauli yake ya ‘Chidi Benz ni mtu wa kuachwa afe’ ambayo ilichuliwa vibaya na baadhi ya wadau imedhihirika hivi karibuni baada ya rappa huyo kudaiwa kutoweka sehemu ambayo alikuwa akipatiwa matibabu ya kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Dudu Baya

Miezi miwili iliyopita katika kipindi kimoja cha runinga, rappa Chidi Benz alikiri kutumia Madawa ya kulevya na kuhitaji msaada ambapo Babu Tale pamoja na Kalapina walimsaidia kwa kumpeleka Bagamoyo Sober House ambako anadaiwa alitoroka siku 28 baadae.

Kupitia instagram, Dudu Baya ameandika:
Habari zilizopo ni kwamba msanii mwenzangu Chidi Benz ametoroka rehab aliyopelekwa ya Bagamoyo sober house. Miezi miwili iliyopita nilifanyiwa mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari pamoja na blogs na websites mbalimbali. Na kila walipokuwa wananiuliza kuhusu swala la Chidi Benz kusaidiwa na Babu Tale kupelekwa rehab, nilikuwa nawajibu kuwa msanii Chidi Benz ni mtu wa kuachwa AFE!! Kwani kwa tatizo alilonalo ni ngumu kwa mtu yeyote (hata mama yake mzazi) kuweza kumsaidia na kupona bila ya yeye mwenyewe Chidi Benz moyo wake haujaridhia kuacha madawa ya kulevya. Baadhi ya wasanii wenzangu, watu maarufu, wanasiasa,wafanyabiashara n.k waliweza kuniponda na kunipinga waziwazi kutokana na kauli yangu hii na waliniona kuwa mimi sio mtu mzuri ninayetaka kumsaidia CHID BENZ apone. Lakini ukweli wa yale maneno niliyosema umekuja kudhihiri hivi majuzi baada ya yeye msanii mwenyewe CHID BENZ kutoroka rehab kwa kukataa kusaidiwa kuondokana na matatizo yake!! So kinachofanyika sasa hivi ni kuweza kumtafuta CHID BENZ sehemu aliyokimbilia ili akipatikana aweze kuludishwa Rehab. Sina tatizo lolote na CHID BENZ na wala simuombi mabaya kwani mimi ni kama kaka yake na huwa ninamuombea kwa Mungu aweze kutoka na kupona haraka kwa haya matatizo yaliyompata. Ila narudia tena kusema kuwa tatizo alilonalo mwenyewe CHID BENZ @chidbenz ni mbaka hapo yeye mwenyewe moyo wake uridhie kuachana na matatizo hayo na sio kuweza kusaidiwa na watu kuondokana na matatizo hayo (CHID BENZ my best rapper hakuna wa kukuokoa, JIOKEE!!) Msaada wangu kwako, naendelea kumuombea.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top