Loading...

HABARI YA HIVI PUNDE: KUTOKA BUNGENI BUNGE LAWAKA MOTO HIVI PUNDE BAADA YA KITIMTIMU CHA WABUNGE MAJANGILI KUTAKIWA KUPIGWA RISASI HUKU MAGIGE NA MAGHEMBE WAKINUKISHA BUNGENI NA KUENDELEA KUZUA HOFU KUBWA KWA WABUNGE HAWA MAJANGILI SHUHUDIA TUKIO HILI HAPA.....

MBUNGE wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM) amesema Bunge linapaswa kufahamu ni mbunge gani ambaye anajihusisha na ujangili, kwani hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria.

Magige, ambaye amependekeza sheria ibadilishwe majangili ama wapigwe risasi au wafungwe jela maisha, ni miongoni mwa wabunge ambao walivalia njuga suala la ujangili jana wakati wakichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.MAGHEMBEKwa upande wake, serikali kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17, alisema majangili nguli wanane wenye mitandao ya kimataifa ni miongoni mwa wahalifu 53 waliohukumiwa baada ya kukutwa na hatia.

Wabunge majangili? Akichangia, mbunge Magige alisema inasemekana baadhi ya wabunge wanajihusisha na ujangili hivyo akashauri ni vyema wakafahamika. “Inasemekana baadhi ya wabunge wanajihusisha na ujangili. Huyo jangili ni nani? Munde Tambwe, Catherine Magige au Ally Keissy,” alihoji mbunge huyo wa Viti Maalumu kutoka Mkoa wa Arusha. “Hakuna aliye juu ya sheria, tunaambiwa majangili tunao humu ndani, tunataka tuwafahamu, tusinyooshee vidole wengine,” aliongeza Magige.

Alisema ujangili umekithiri nchini na tembo wanatoweka. Alipendekeza sheria ibadilishwe majangili ama wapigwe risasi au wafungwe jela maisha. Majangili nguli watajwa Profesa Maghembe alisema katika mwaka 2015/16, doria zilifanyika ndani na nje ya Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu kwa siku-doria 109,474 na ziliwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 1,176 na kesi 654 zilifunguliwa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top