Loading...

Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania limeguswa na hujuma kwa Rais Magufuli

Mei 8 2016 Jukwaa huru la Wazalendo Tanzania limekutana na Waandishi wa Habari Dodoma ili kutoa tamko lao kuhusu hujuma dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

Katibu wa jukwaa hilo Mtela Mwampamba amesema
’Kwa miaka mingi Watanzania tumekuwa tukipiga kelele tukilia juu ya kero mbalimbali za Serikali kushindwa kupambana na watumishi wasio wema na wabadhirifu, mafisadi, wala rushwa na wahujumu uchumi‘

‘Vita hii tumekuwa tukipigana sisi wanyonge na baadaye ikaungwa mkono na makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, Sasa tumempata Rais Magufuli anayefanya kazi bila kuchoka kuifikisha Tanzania tunakokutaka, wanasiasa hao wamegeuka na wanaanza kumhujumu‘

‘Tumeshangazwa zaidi tunaposoma na kusikia katika vyombo vya habari baadhi ya wanasiasa wakianza kumkejeli Rais Magufuli eti anaendesha nchi kinyume cha sheria na kuipeleka katika utawala wa kiimla‘

‘Ni kwasababu hii, sisi wazalendo tunasema hoja za wanasiasa na wasomi kusema Rais analeta utawala wa kidikteta kwa kutumbua majipu tunaona ni hali zilizojaa hisia binafsi na zaidi ujasiri wa hujuma‘

Mwampamba hajaacha lipite hili la Sukari, nalo anasema…>>’Baadhi ya wafanyabiashara kuficha badhaa muhimu ya sukari, tunatumia fursa hii kuwakumbusha kuwa waachane na hujuma hiyo mara moja.‘

‘Wanaoendesha uhujumu huo wa uchumi ni sawa na hawa wanasiasa wanaoendekeza hujuma dhidi ya Rais Magufuli ili asiendeleze mageuzi ambayo Watanzania wenyewe waliyataka na wameyasubiri kwa muda mrefu‘

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top