Loading...
Home »
Unlabelled »
LAKUZINGATIA UKITAKA KOLABO NA BARAKA DA PRINCE
Kushirikiana ni jambo la msingi sehemu yoyote bila ushirikiano mambo hayawezi kwenda, kauli za Alikiba na Diamond katika mahojiano mbali mbali walisikika wakisema kuwa msanii akitaka”Collabo” lazima ajitathimini kwanza ndio wafanye “Collabo” hii inathibitisha kuwa Collabo ina umuhimu mkubwa kwa msanii.
UFAFANUZI WAO
Kwanini wametoa kauli hizo? walimaanisha kuwa msanii mchanga anapo taka ushirikiano katika nyimbo lazima ajipange na uwezo binafsi sio pesa uwezo wake ndio utambeba ili ngoma iwe kali, ikiwa msanii ana uwezo mdogo wanahofia kumfunika msanii huyo na haita msaidia kwani lengo la msanii mchanga ni kutoboa katika ramani ya muziki.
BARAKA DA PRINCE ANA YAKE
Kupitia Clouds Fm XXL amesema kuwa anapata simu nyingi kwa wiki zinazo mtaka afanye Collabo inawezekana asikubali hata moja kutokana na uwezo binafsi wa msanii wengine wakimtaka wampe pesa ili wafanikishe ushirikiano huo hivyo ame waomba wajipange kama maneno ya kaka zake .
Baraka Da Prince anatarajia kutoa nyimbo aliyo mshirikisha Ali Kiba huku nyimbo aliyofanya na Mr Blue pamoja na Ben Paul ziko hewani.
Tuesday 3 May 2016
Post a Comment