Loading...

Magufuli: Siwezi Kulipa Tshs Bilioni 60 za TPI Zilizoamriwa na Mahakama



Rais Magufuli amesema kuwa hatothubutu kulipa tozo ya Tshs bilioni 60 kama fidia kwa TPI kufuatia kushinda kesi mahakamani.

Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI ) kinachomilikiwa na wadau wa tatu akiwemo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ndugu Ramadhan Madabida walizuiwa kufanya shughuli za uzalishaji kwa miaka minne sasa kufuatia hatia dhidi ya mfamasia wa kiwanda hicho bi Zarina Madabida za kuzalisha ARVs feki.

Hata hivyo TPI walishinda shauri hilo na kufungua kesi ya madai ambayo walishinda.

Ikiwa deni hilo litadumu tena kwa miaka miwili ijayo linaweza kuigharimu zaidi serikali

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top