Loading...

'Makonda awatundikia kitanzi viongozi Dar watumishi hewa


Makonda amechukua hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya watumishi wa manispaa tatu za Ilala, Kinondoni na Temeke, jijini humo, iliyowasilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dar es Salaam, Theresia Mbando .
Hata hivyo, wakati wa baada ya kusaini mikataba hiyo, baadhi ya wakuu wa idara walionekana kutoridhika kwa kutonyanyua mikataba yao juu, huku wengine wakinyanyua kwa kutokujiamini.
Makonda alisema mkoa wa Dar es salaam unawatumishi wa serikali walio chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi 26,324, ambao kati yao 166 ni wa Sekretarieti ya Mkoa na 26,158 ni wa mamlaka za Serikali za mitaa, kutoka halmashauri ya jiji 254, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala 8710, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni 9009 na Halmashauri ya Temeke 8,185.
“Jumla ya watumishi 26,115 wameshahakikiwa sawa na asilimia 99.2, kati yao 209 wamebainika hawastahili kuwapo katika orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi hewa ambao walilipwa jumla ya Sh. 2,91,452 304.82,” alisema.
Alisema kila idara inawatumishi hewa, hivyo wakuu wa idara wote wasaini mikataba itakayo onyesha kila idara ina watumishi hewa wangapi na halali wangapi waliopo katika halmashauri zao.
Hata hivyo, kwa upande wa wakuu wa idara shughuli hiyo ilionekana kuwa gumu baada ya kuibuka sintofahamu ya kutojuwa kwa uhakika wanawatumishi hewa wangapi katika halmashauri zao.
“Sitaki yanikute kama yaliomkuta mama yangu Anne Kilango Malechela (aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga), maana ninyi wakuu wa idara mnatoa taarifa zisizo sahihi na kumfikia mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na hatimae Rais,” alisema.
Kwa upande wa wakuu wa idara, walitaka kupewa ufafanuzi wa mikataba hiyo. Mwalimu Ngonyani wa Manispaa ya Ilala alitaka kujua kama watumishi waliopo vyuoni bila ruhusa wawekwe katika watumishi hewa au la, lakini swali lake halikupatiwa ufumbuzi .
Makonda alisema idara atakae idhinisha mshahara wa watumishi hewa atalazimika kulipa gharama zote za serikal na atachukuliwa sheria za kinidhamu na kufukuzwa kazi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top