Loading...

BREAKING NEWS: TUKIWA BADO TUPO KATIKA STORI ZA KITWANGA NA SHTUMA ZAKE ZA ULEVI SASA RAIS MAGUFULI KUFANYA UTEUZI MMWINGINE HIVI PUNDE HUU SASA NI UTEUZI MADHUBUTI KABISA KUTOKA IKULU....

IMG-20160523-WA0007

Rais Dk. John Magufuli amemteua Gerson Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imesema kabla ya uteuzi huo, Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri ambapo anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top