Mtoto wa Kitanzania Getrude Clement mwenye umri wa miaka 16 kutoka Mwanza, aliwahutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa, New York Marekani kuhusu mabadiliko ya tabianchi, wakati nchi 175 zilipokutana kusaini makubaliano ya Paris.
Mei 2 2016 Getrude alipata nafasi ya kufika bungeni Dodoma baada ya kupewa mwaliko wa Serikali, nje ya Bunge kakutana na Waandishi wa habari na kusema…>>>’Nimejisikia vizuri sana kufika katika Bunge la Tanzania, ni mara yangu ya kwanza na nimejihisi nimepata heshima ya kipekee‘
‘Niliweza kuhudhuria katika baraza kuu la umoja wa mataifa April 22, Tanzania katika utunzaji wa mazingira hata mvua ikinyesha unaweza usitamani kutoka hata nje‘
Nini tofauti alizojifunza kati ya Marekani na Tanzania?…>>>’Tofauti nilizoziona kati ya Marekani na Tanzania nimeona kwanza wenyewe wana viwanda vingi lakini maeneo yao ni masafi sana, maisha ya kule ni tofauti na ya kwetu, huku tunaishi kwa kushirikiana lakini kule kila mtu yupo kivyake‘
Kwa upande wa Profesa Anna Tibaijuka anasemaje akiwa kama mzoefu na masuala ya Umoja wa Mataifa?…>>>’Kwanza Taifa limeweza kutoa mtoto mwenye kipaji na utaratibu wa shule za kata ambazo yeye mwenyewe pia amesoma zinaweza sasa kuonyesha vipaji‘
‘Umoja wa Mataifa wanatuona sisi na ndiomaana wanatukaribisha ili kuondoa hali ya ubaguzi na mazingira kandamizi ambayo huwa yanadidimiza viapaji vya watu hasa katika nchi zinazoendelea‘
Post a Comment