Loading...
Home
»
NEWS
»
BREAKING NEWS: MKANGANYIKO MKUBWA UMEIBUKA TENA NDANI YA CCM RAIS MAGUFULI KUFANYIWA MIZENGWE YA AJABU NA VIGOGO HAWA KIGOGO HUYU AFUNGUKA A TO Z ZIDI YA FIGISUFIGISU ANAZOFANYIWA RAIS MAGUFULI...
Hivi karibuni niliandika makala yenye kuhoji kama Rais Magufuli atapokea kijiti cha Uenyekiti wa CCM Taifa kutoka kwa Mwenyekiti wa sasa Dk. Jakaya Kikwete mapema kama inavyosemekana; tayari baada ya vigogo wameanza kutifuana ndani ya chama hicho na kugawanyika wakihofia ‘kutumbuliwa’ kwani ni dhahiri chama hicho kimelea majipu sugu kwa kipindi kirefu.
Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema baadhi ya vigogo wameanza kufanya figisufigisu ili Rais Magufuli achelewe kukabidhiwa kijiti hicho kwani inaonesha dhahiri shahiri atasambaratisha majipu sugu yaliyokitesa na kukivuruga chama hicho kwa siku nyingi.
Mmoja wa viongozi wa juu wa chama hicho ambaye anaimani kubwa na Rais Magufuli ya kuendelea kutekeleza kile ambacho chama kimekuwa kikitamani kufanya lakini kikakwamishwa na wachache walio na maslahi binafsi, anaamini hivi sasa Rais Dk. Magufuli anatekeleza tena kwa vitendo jambo linalowanyima usingizi vigogo wasio waadilifu ndani ya chama hicho huku wakitamani asikabidhiwe Uenyekiti hivi sasa.
Katika Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC), kilichoketi hivi karibuni Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, taarifa zinasema mpaka sasa haijajulikana tarehe rasmi ya Mkutano Mkuu maalumu uliopangwa kufanyika Juni mwaka huu ili kufanya makabidhiano rasmi ya chama, kutokana na Rais Magufuli kuundiwa zengwe ili achelewe kukabidhiwa nafasi hiyo.
Filed Under:
NEWS
Thursday 5 May 2016
1 comments:
Ukiona kuna zengwe ujue kweli Rais JPM anasimamia haki
ReplyPost a Comment