Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Tawala Bora, Angela Kairuki amewataka wahitimu wa Chuo cha Utumishi Umma nchini (TPSC) kutojihusisha na masuala ya ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kazini badala yake wawe wachapakazi watakapowatumikia Watanzania.
Kairuki alitoa kauli hiyo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomwakilisha waziri huyo kwenye mahafali ya 24 ya chuo hicho yaliyofanyika tawi la Mbeya.
Alisema wakati Serikali ya awamu ya tano ikiendelea kupambana na watumishi hewa, mafisadi na wazembe kazini, wahitimu katika chuo hicho wahakikishe wanakwenda kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za utumishi popote watakapoajiriwa.
“Huu ni wakati wenu kuonyesha utofauti kati ya aliyehitimu chuo na kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, yule ambaye hajapitia chuo chochote, lakini yupo ofisini utendaji kazi wake unadhihirisha kuwa hakustahili kuwapo mahali hapo,” alisema.

Post a Comment