Ofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Amani Mkwizu na mfanyakazi wa kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Edward Magobela wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashtaka matatu ya rushwa.
Washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo wakidaiwa kuomba rushwa ya Sh50 milioni nyingine Sh5 milioni na kupokea rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Commercial Sales and Services Tanzania Limited, Glenn Clarke.
Akiwasomea mashtaka washtakiwa hao, Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Denis Lekayo aliliieleza mahakama kuwa washtakiwa waliomba na kupokea kiasi hicho cha pesa kama rushwa ili kumwezesha kumpunguzia kodi aliyokuwa anadaiwa kutoka Sh375 milioni hadi Sh100 milioni.
Hata hivyo washtakiwa hao walikana mashtaka yote na upande wa mashtaka ulisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Post a Comment