Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC),Bi. Juliet Kairuki kuanzia tarehe 24.4 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari na katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, imesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya rais Magufuli kupata taarifa kuwa Mkurugenzi huyo alikua hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiliwa mwaka 2013 hatua ambayo rais amezua maswali mengi.
Aidha Taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu huyo imeongeza kuwa endapo Bi. Kairuki atakuwa tayari kuendelea kufanyakazi na Serikali ya awamu ya tano atapangiwa kazi nyingine huku mchakato wa kumpata Mkuregenzi mpya umeanza mara moja.
Kwa mujibu wa Prof. Mkenda kwenye taarifa yake hiyo amesema Bw. Clifford Katondo Tandali, atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho cha uwekezaji nchini TIC.
Post a Comment