Instagram siku hizi kimekuwa ni kiota cha umbea wa mjini, Alhamisi hii akaunti moja maarufu ya umbea imeweka picha ya mwanadada anayedaiwa kuwa ni mpenzi mpya wa mbunge wa Mbeya, Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ pamoja na gari ambalo anadaiwa kuzawadiwa siku yake ya kuzaliwa.
Akaunti hiyo ilipost picha (hapa juu) na kuandika:
Sugu shikamooo!ahsante kwa kutunyoosha sio kwa bday zetu zile za kiingilio na za kusaka wafadhiri miezi 3!kha hilo lizawadi toka kwa baby ni funga kazi..mtatoo umetulia hata ukiachwa huna haja ya kufuta bana raha si ulishazila bana?? jamani wagonjwa wanaendeleaje huko ICU??…Ukishindana na moto lazima ukuunguze dadeki
Post hiyo ina komenti tofauti tofauti ambapo baadhi ya mashabiki waliamua kumtag mpenzi wa zamani wa Sugu, Faiza Ally ambaye alizaa naye mtoto mmoja aitwae, ‘Sasha’.
Faiza Ally ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi aliamua kujibu na kuandika:
Mmnanitag ili iweje ? watu wamenunuliwa magorofa kariokoo itakua harrier people grow up!
Post a Comment