Nusu fainali ya Kombe la Azam Sport Federation Cup kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga imevunjika kwa sababu ya mashabiki wa Coastal Union kuleta vurugu kutokana na kutoridhishwa na uchezeshwaji wa mchezo huo, muamuzi akaamua asimamishe mpira ikiwa inaelekea dakika ya 105 kabla ya kuzimaliza dakika 120, wakati ambao Yanga walikuwa mbele kwa goli 2-1.
Baada ya mchezo huo kuvunjika uliyokuwa unarushwa Live kupitia Azam Tv, ripota wa Azam Tv alifanya mahojiano mafupi ya Live kutoka katika uwanja wa Mkwakwani Tanga na kaimu mkurugenzi wa mashindano wa TFF Jemedali Said ilikujua mambo yatakuwaje mchezo utarudiwa au inakuwaje?
“Kiukweli mchezo umevunjika lakini haya mashindano yanaendeshwa kwa kanuni na taratibu ila sisi tunasubiri ripoti ya muamuzi na kamisaa wa mchezo ili tuweze kufanya maamuzi” Jemedali Said
Post a Comment