Msanii Mo Music ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa 'Skendo' amefunguka na kusema kuwa kwa sasa amechoka kusema uongo na kuwadanganya mashabiki zake juu ya kazi zake na ukimya wake kwenye muziki.
Mo Music akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana alidai kuwa mara nyingi amekuwa akitoa ahadi zisizo timia kwa mashabiki wake kutokana na menejimenti yake kushindwa kazi yake, ikiwepo kumfanyia video pamoja na jambo ambalo limekuwa likimkwamisha na kumrudisha nyuma.
"Unajua uongozi wangu umefika sehemu ambayo kwa sasa kwangu kuvumilia imekuwa ni ngumu kwa sababu mwanzo walinichukua kama ndugu na tuliishi kama ndugu, kwa sasa nimefanya nao kazi huu mwaka wa tatu mimi napiga jalamba lakini sioni mafanikio yoyote kiuchumi, na mimi saizi ni majukumu mengi kuna watu wanasoma kwa ajili yangu mwenyewe natakiwa kuendesha maisha kwa kazi hivyo kazi zinapokuwa haziendi nazidi kukwama mimi" alisema Mo Music.
Mbali na hilo Mo Music anasema alifika hatua aliamua kufanya maamuzi magumu na kuwashirikisha wanafamilia wake na kuamua kwenda kuonana na uongozi wake ili yeye aendelee na kazi zake mwenyewe baada ya kuona hakuna jambo lolote ambalo linafanywa na uongozi wake huo katika kuhakikisha msanii huyo anazidi kusonga mbele.
"Unajua hata mimi nimechoka kusema uongo mbele za mashabiki zangu, kila siku mimi nilikuwa nikimfuata meneja wangu juu ya kufanya video ananiambia waambie tutafanya wiki ijayo so nilichoka na hali hiyo ya kusema uongo kila siku, ndiyo maana unaona mpaka sasa sina video ya kazi zangu kadhaa kwa sababu uongozi ulikuwa hauna uwezo wa kuendelea kunipeleka mbele zaidi, ndiyo maana unaona hata mzunguko wa nyimbo zangu kwenye vyombo vya habari ulikuwa unapungua siku hadi siku na mambo mengi kwenye muziki wangu yalikuwa yanakwama kwa sababu ya uongozi".
Kutokana na hali hiyo, Moe anaweka wazi maamuzi aliyoamua kuchukua kwa kusema "Kwa sasa nimeamua kwenda mwenywe sina uongozi na imani yangu nitasonga mbele zaidi kwani Mungu aliyenipa kipaji na mashabiki ndiyo wamefanya mimi kuwa Moe Music hivyo bila hata ya uongozi wa Aljazeera Entertainment imani yangu nitaweza kusimama na kusonga mbele zaidi.
Post a Comment