Loading...

Vituko Kumi Ambavyo Havitasahaulika vya Marehemu Lucy Kibaki...

 IJUMAA iliyopita uvumi ulienea kuhusu mahali alikokuwa Mama Lucy Kibaki, aliyekuwa mke wa rais mstaafu wa Kenya,  Mwai Kibaki, ambapo vyombo vya habari vilieleza kwamba alikuwa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali moja jijini Nairobi.

Mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 75 alikuwa haonekani sana hadharani tangu mwaka 2010 na kutokuwepo kwake kulionekana wazi baada ya kutohudhuria hafla ambapo mumewe, Rais Kibaki, alikabidhi madaraka kwa Uhuru Kenyatta mwaka 2013.

Yote kwa yote, taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya Rais Uhuru Kenyatta ilisema mama huyo alifariki jana katika hospitali moja jijini London, Uingereza, alikokuwa anapatiwa matibabu na kwamba mipango ya mazishi yake ilitegemewa kutangazwa baadaye.
Lucy
Yafuatayo ni matukio kumi ambayo yalimhusisha mama huyo ‘mcharuko’ aliyekuwa hawezi kujizuia anachotaka kukisema ama kukifanya:


  • Miezi kadhaa baada ya mumewe kuapishwa kuwa rais wa tatu wa Kenya, alisemekana aliifunga baa iliyokuwa ndani ya Ikulu ambapo mawaziri na marafiki wa karibu wa Mwai Kibaki walikuwa wanaitumia kwa kujiburudisha na kiongozi huyo mpya wa nchi.
  • Aliwahi kumwambia mumewe aitishe mkutano wa dharura wa waandishi wa habari Ikulu na atangaze waziwazi kwamba hakuwa na mke mwingine zaidi yake. Hii ni baada ya kuwepo uvumi kwamba alikuwa na mke wa pili.


  • Mnamo Mei 2005, aliingia ndani kwa jirani yao, mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini humo, Makhtar Diop, akiwa amevaa suti la michezo (tracksuit) usiku wa manane na kumtaka afunge au apunguze sauti ya muziki aliokuwa anaupiga. Bw. Diop siku hiyo alikuwa ana sherehe ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Kenya.
  • Baada ya tukio hilo kwa Bw. Diop, magazeti yaliliandika sana, jambo lililomfanya mama huyo kuzivamia ofisi za Nation Centre, ambazo ni ofisi za kampuni ya vyombo vya habari vya Nation Media Group, Mtaa wa Kimathi, na akataka mwandishi aliyeandika habari kuhusu mgongano wake na Bw. Diop akamatwe.Lucy Kibaki 2
  • Mama huyo alikuwa ni mtu wa kwanza miongoni mwa watu maarufu kumtwanga mwandishi; alifanya hivyo kwa kumzaba kibao mpiga picha Clifford Derrick aliyekuwa akimpiga picha baada ya kuingia kwa vishindo ofisi za Nation Centre.
  • Vituko vyake havikuishia hapo. Kuna wakati alimchapa kibao mshereheshaji (MC) kwenye sherehe za Siku ya Jamhuri mwaka 2007 zilizofanyika Ikulu.  Mshereheshaji huyo alifanya kosa la kipumbavu alipomtambulisha mke wa rais kwa jina la Lucy Wambui badala ya Lucy Muthoni Kibaki.lucy akidondoka kwenye ngazi

Wakati wa sherehe za Siku ya Jamhuri mwaka 2009 zilizofanyika Uwanja wa Nyayo, mama huyo aliteleza na kuanguka kwenye ngazi lakini akasaidiwa kwa kuinuliwa na walinzi wake.

  • Katika kuendeleza vituko, anasemekana alimzaba kibao mfanyakazi wa Ikulu, Matere Keriri, ambapo mfanyakazi huyo alikuja kueleza mwenyewe kwamba mke huyo wa rais alikuwa hajisikii vizuri kwa yeye (Keriri) kuwa na ukaribu sana na rais.
  • Katika miaka yake kumi aliyokuwa Ikulu alikuwa hawezi ‘kumechisha’ nguo zake na hafla husika. Siku aliyofanya kioja kikubwa zaidi cha tabia hiyo ni pale alipovaa gauni la rangi ya samawati (bluu) kwenye chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais George W. Bush katika Ikulu ya Marekani. Gauni hilo lilikosolewa sana na watu Wakenya kutokana na kitambaa chake kuwa cha bei rahisi na likiwa katika ‘dizaini’ ambayo haikuufanya mwili wake upendeze.
  • Lucy Kibaki anasemekana pia alimzabua kibao mwanasheria na mwanasiasa, Gitobu Imanyara, katika hafla kuhusu masuala ya bunge iliyofanyika Ikulu. Mama huyo anasemekana alichukizwa na pale mwanaasiasa huyo alipokuwa anasisitiza kwamba kumfungulia mashitaka mbunge mmoja aliyekuwa amemshambulia kwa maneno rais (Kibaki) ni kupoteza muda.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top