Loading...
Home »
Unlabelled »
BI CHEKA KULA MAFAO YA TMK
Kulingana na desturi na kanuni za jamii za Kiafrika aghalabu mtu mzima anapofika umri mkubwa huwa anatulia nyumbani kwa ajili ya kupunzika na pilikapilika za maisha na kuwapisha vijana ambao damu inachemka ili kulisongeshe gurudumu la maendeleo ya taifa huku wazee wakiachwa wazifaidi ‘Pension’ zao baada ya kumaliza majukumu ya ujenzi wa taifa ambapo msanii wa muziki hapa nchini Bi. Cheka amekutwa na hali hiyo.
Kupitia kundi la Mkubwa na Wanawe Mwakilishi na Msanii wa kundi hilo Mh. Temba amesema kwa sasa Bi Cheka anapaswa kupumzika hasa kutokana na umri na afya yake kwani aliwahi kuanguka jukwaani mara mbili kwani ni wazi umri wa msanii huyo umekwenda.
MAISHA BAADA YA KUSTAAFU
Kupitia XXL ya Clouds Fm Temba amefunguka na kusema kwa kutambua mchango wa msanii huyo katika kundi hilo, kuanzia sasa chochote kitakachopatikana Mkubwa na Wanawe Bi Cheka atapewa ili kukidhi mahitaji yake ya nyumbani.
Tuesday, 3 May 2016
Post a Comment