Jina la aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda Ukawa, jana liliingia tena katika Bunge la Kumi na Moja na kuzua mvutano.
Lowassa alitajwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), wakati akijibu hoja za Mbunge wa Kibamba, John Mnyika aliyekuwa akihoji na kuonesha kushangazwa na uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati alijiuzulu bungeni hapo baada ya kuelemewa na kashfa ya akaunti ya ‘Tegeta Escrow’.
Akijibu hoja hizo, Keissy ambaye siku zote ni mbunge mwenye hoja machachari alimvaa Mnyika na kuhoji mbona wao ( UKAWA) walimchukua Lowassa na kumfanya kuwa mgombea wao wa Urais wakati alijiuzulu uwaziri Mkuu kwa kashfa ya Richmond.
“Mnabeza uteuzi wa Muhongo wakati Lowassa alivyojiuzulu hapa hapa bungeni mlimchukua mkamtembeza nchi nzima. Leo angekua Rais mgesema nini?” Alihoji Keissy .
Mnyika alikuwa alisoma hatuba ya kambi ya upinzani kwa Wizara ya Nishati na Madini ambayo ilikuwa ikiponda uteuzi wa Profesa Muhongo
Post a Comment