Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea kabla ya mwisho wa mwaka huu katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Hayo yamebainika Ikulu jijini Dar es Salaam wakati Rais John Magufuli alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke na Balozi wa Denmark nchini Eina Hebogrd.
Kiwanda hicho cha kuzalisha mbolea kinachotarajiwa kujengwa wilayani Kilwa mkoani Lindi kitatumia rasilimali ya gesi asili na miamba ya matumbawe iliyopo wilayani humo na kitajengwa kwa ubia kati ya Tanzania na nchi za Denmark, Ujerumani na Pakistani na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 3,800 za mbolea kwa siku.
Wakati wa mazungumzo baina ya Rais Magufuli na Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke na Balozi wa Denmark nchini Eina Hebogrd mabalozi hao wamesema kiwanda hicho kikubwa barani Afrika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mbolea itakayotosheleza mahitaji ya wakulima wa Tanzania na nyingine kuuzwa nje ya nchi na kuzalisha ajira zaidi ya 5,000 na uwekezaji wake utagharimu Bilioni 3 za Kimarekani.
Rais Magufuli amewaahidi mabalozi hao kuwa serikali yake itatoa ushirikiano wa kutosha kuharakisha utekelezaji wa mradi huo.
Filed Under:
NEWS
Saturday, 21 May 2016
1 comments:
Hii ndio Tanzania ya viwanda tunayoitarajia
ReplyPost a Comment