Loading...
Home
»
NEWS
»
BREAKING NEWS: KAULI YA RAIS MAGUFULI YA JULAI 15 YAWA GUMZO JIJINI LONDON WAINGEREZA WATAHAMAKI NA JITIHADA ZAKE WANENA HILI ZITO MAJALIWA AFUNGUKA MAKUBWA ZAIDI
Katika kampeni za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Magufuli alijiapiza kwa Watanzania kama watamchagua kuwa Rais wa Tanzania basi mafisadi na wanaohujumu uchumi wa nchi waanze kutubu kwani hatawavumilia.
Julai 15 mwaka jana katika Viwanja vya Jangwani wakati wa kampeni Rais Magufuli alisema “Ninazungumza jua linawaka haki ya MUNGU kweli tutafanya kazi, niwaombe tushikamane kwa pamoja sura yangu ni mbayambaya lakini saa nyingine inakuwaga nzuri usiku, sura ya tabia ni nzuri lakini mnachohitaji ni kazi, maendeleo na kuondolewa kero zenu.. mimi sio mkali ila nawachukia watendaji ambao hawatimizi wajibu wao, mafisadi na majizi hao nitalala nao mbele”.
Mara baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani alianza mara moja kushughulikia mafisadi na wabadhilifu wa mali za umma ambapo katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Rushwa viongozi wakuu wa nchini na washiriki wa mkutano huo wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua katika kukabiliana na ufisadi pamoja na rushwa.
Katika mkutano huo uliofanyika jijini London, Uingereza ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais Magufuli alivitaja vigezo vilivyoipaisha Tanzania ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalumu ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai mwaka huu, mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za watoa taarifa.
Filed Under:
NEWS
Saturday, 14 May 2016
Post a Comment