Loading...
Home
»
NEWS
»
BREAKING NEWS: LEO NI HISTORIA MPYA NA YA AINA YAKE KWA MARA YA KWANZA TANZANIA HUU NDIO UTEUZI WA MTOTO WA MKULIMA ULIOFANYIKA HIVI PUNDE NA RAIS MAGUFULI SHUHUDIA UTEUZI HUU HAPA KUTOKA IKULU...
Kwa mtazamo wa haraka haraka ni kama vile nyota za Mawaziri Wakuu Wastaafu kila mara zimeendelea kung’ara hapa nchini na sababu huenda ikawa ni uwezo wao katika utendaji uliofanya jamii ithamini na kuuona mchango wao.
Jaji Joseph Sinde Warioba aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa Tano enzi za utawala wa Mzee wa Ruksa, Ally Hassan Mwinyi, baada ya kustaafu amekuwa na mchango mkubwa kwa taifa na ndiye aliyefanikisha zoezi la kupata Rasimu ya Kwanza na ya Pili ya Katiba Inayopendekeza.
Mawaziri Wakuu Wastaafu Frederick Sumaye na Edward Lowassa baada ya kulitumikia taifa sasa wametimkia upinzani na hivi sasa wanafanya jitihada ya kukijenga Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania Bara cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Baada ya kukalia kiti cha Uwaziri Mkuu kwa takribani miaka 7, leo bahati imemwangukia mtoto wa Mkulima, Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mizengo Pinda, baada ya kuteuliwa na Rais Dk. Magufuli kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Itakumbukwa Januari 21 mwaka huu Rais Magufuli alimteua Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, taarifa iliyotolewa leo na Ikulu imesema Pinda anachukuwa nafasi iliyoachwa na Dk. Asha- Rose Migiro ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Filed Under:
NEWS
Wednesday, 25 May 2016
Post a Comment