Loading...

BREAKING NEWZ…(VIDEO) RAIS MAGUFULI KIBOKO AMUWADHIBU VIKALI MKE WA WAZIRI WA MAMBO YA NJE (MAHIGA) NA KUMPANDISHA CHEO TRAFFIC ALIYEMKAMATA MKE WA WAZIRI HUYO

john-magufuli
Inasemekana kwamba Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje Tanzania, Mama Mahiga alimtukana askari wa usalama barabani baada ya dereva wa mama huyo kutenda kosa. Tukio hilo ambalo taarifa yake ilifika mezani kwa Mheshimiwa Rais John Magufuli limemfanya Rais kuamuru trafiki huyo kupandishwa cheo huku akisisitiza hakuna mtu aliye juu ya sheria. Bonyeza na kuyasikiliza maongezi ya simu kati ya trafiki huyu na mkuu wake wakati akiripoti tukio hilo.
SIKILIZA HUYU MAMA AKIJIBISHANA NA TRAFIC
Chini ni Video ya maoni ya Rais Magufuli kuhusu tukio hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Kamishna wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernesti Mangu kumpandisha cheo askari wa Usalama barabarani ambaye alitukanwa na Mke wa Waziri wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi.

Rais ameyasema hayo wakati akifungua Kikao cha Makamanda wa Polisi wa Mikoa. Aidha Rais Dr. Magufuli amesema ameshamuonya Waziri huo ambaye mke wake amemtukana askari wa Usalama Barabarani.



Wakati akitoa agizo hilo, rais amesema hakuna kiongozi au familia ya kiongozi iliyoko juu ya sheria.

Chanzo: TBC1

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top