Loading...
Home
»
MATUKIO
»
NEWS
»
HABARI YA HIVI PUNDE: HII NI KUTOKA BUNGENI BUNGE LAZIDI KUSHIKA KASI MAJI MAREFU AWALIPUA WABUNGE HAWA NA KASHFA NZITO YA NHC NA KUZUA TAHARUKI YA AINA YAKE.....
MBUNGE wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (CCM), maarufu kwa jina la ‘Maji Marefu’ amewalipua wabunge waliokosa ubunge katika kipindi hiki na vilivyopita kwa kuhodhi nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mjini hapa na kupangisha watu wengine kinyume cha utaratibu wa shirika Alisema hali hiyo imefanya wabunge wapya, ambao ni asilimia 70 ya wabunge wote kwa sasa, kukaa nyumba za kulala wageni wakati zipo nyumba hizo kwa wabunge kulingana na mkataba na NHC.
Mbunge alisema wapo watu wamepangishwa na wabunge hao wa zamani, ambao wamegeuza nyumba hizo kama kitega uchumi kinyume na taratibu. Ngonyani alisema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Alimuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kufuatilia suala hilo na shirika kwa ujumla, aondoe wapangaji hao waliowapangishia wengine kinyume cha utaratibu na kuwapatia nyumba wabunge wapya ambao hawana nyumba za kuishi.
Alisema wabunge hao waliokosa nafasi ya kurudi jimboni miaka tofauti, mkataba wao wa kupangishwa nyumba hizo umekwisha, kwani ukishakosa ubunge hauna dhamana tena mpaka utakaporudi.
“ Kuna wapangaji wengi ambao ni wabunge waliokosa nafasi hiyo ambao wamepangishwa na shirika na badala yake hadi leo wamezishikilia nyumba hizo hawataki kuziachia, ”alisema Ngonyani.
Post a Comment