Wakizungumza na Enewz kwa nyakati tofauti Petiti alisema kuwa yeye bado ni Manager wa msanii huyo lakini Mirror akikana kuendelea kusimamiwa na Manager huyo huku tukiona katika akaunti yake ya instagram amebadili jina la Mirror na kuweka wasanii wengine.
Kwa upande wa Mirror ameiambia Enewz kuwa Petiti anakusanya pesa kwa wadau kwaajili ya kazi zake lakini hafanyi kazi badala yake anatumia kwa matumizi yake binafsi huku akiongeza kuwa kisa kikubwa cha kutosimamiwa na yeye ni baada ya kumuona akijishughulisha na wasanii wengine.
Post a Comment