Ndege ya abiria iliyokuwa na watu 62 imeanguka ilipukuwa ikitua katika mjini ulio kusini mwa Urusi wa Rostov-on-Don.
Hakukuwa na manusura kati ya abiria 55 na wahudumu saba waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo aina ya Boeng 737 iliyokuwa ikitoka Dubai ilimilikiwa na shirika la Flydubai.
Ndege hiyo ilizunguka kwa karibu masaa mawili kabla ya kufanya jaribio la pili la kutua kufutia hali mbaya ya hewa.
Ilianguka mita mia kadha kutoka kwa barabara ya uwanja ambapo ilivunjika na kushika moto.
Post a Comment