Loading...

Nigeria: Wazazi wa Chibok kwenda Cameroon

Image copyrightAFP
Image captionNigeria: Wazazi wa Chibok kwenda Cameroon
Serikali ya Nigeria inawapeleka nchi jirani ya Cameroon baadhi ya wazazi wa wale wasichana waliotekwa nyara wa Chibok ,kurajibu kuthibitisha iwapo msichana mmoja anayesemekana alikuwa ametumwa kujilipua ni miongoni mwa wanafunzi waliotekwa nyara Chibok.
Msichana huyo alipokamatwa jana alisema yeye ni miongoni mwa wasichana wa Chibok 270 waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram hapo 2014.
Msichana mwengine aliyekuwa pamoja naye wakiwa wamejifunga vilipuzi pia amezuiliwa.
Image captionBoko Haram wamekuwa wakitumia walipuaji wa kujitolea muhanga wa kike katika kampeini yake ya kuzindua himaya yao Kaskazini mwa Nigeria.
Serikali ya Nigeria imesema kuwa inapeleleza madai ya wasichana hao.
Kundi la wanamgambo wa Kiiislamu wa Boko Haram wamekuwa wakitumia walipuaji wa kujitolea muhanga wa kike katika kampeini yake ya kuzindua himaya yao Kaskazini mwa Nigeria.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top