Akiongea kwenye PlanetBongo ya East Africa Radio, Bob Junior amesema aliamua kuwasaidia kwa kuwa aliona ni wasanii wenye vipaji, na yeye alikuwa na vifaa na studio, na ujuzi wa kutengeneza beats.
“Kina Diamond niliwatoa kishkaji tu, unajua niliona wana kipaji,halafu unakuta mtu ana vifaa na studio, hivyo nikaamua kuwafanyia kazi kishkaji kabisa”, alisema Bob Junior.
Pia Bob Junior amezungumzia ukimya wake wa muda mrefu bila kutoa kazi yoyote mpaka sasa alipokuja kuachia wimbo wake na Jose Chameleon wa Uganda, na kusema kuwa alikuwa anajipanga vizuri na kwa sasa watu watarajie kazi za mfululizo kutoka kwake.
“Sasa hivi nimerudi kama unavyoona nina ngoma hiyo na Jose Chameleon, hata hiyo nimeichelewesha kumpisha Barnaba Clasic baada ya kuona naye anaachia ngoma na Chameleon, ila kwa sasa watu wajiandae kila baada ya miezi mitatu nitakuwa naachia ngoma mpya”, alisema Bob Junior.
Post a Comment