Loading...

BREAKING NEWS: MBUNGE ASIEKAUKIWA MANENO BUNGENI BASHE BAADA YA KUWAITA WANAFIKI CCM AZIDI KUISASAMBUA CCM MSILIZE TENA HAPA....

BASHE

Mbunge wa Nzega Mjini Hussen Bashe amesema Bungeni kwamba wabunge na serikali nzima wana wajibu wa kutatua kero za wananchi na wakishindwa kufanya hivyo hakuna haja ya kuendelea kuwa madarakani.

Bashe ameyasema hayo kwa kuwakumbusha wabunge hotuba ya Rais wa awamu ya kwanza Mwl. Julius Nyerere ambaye alisisitiza uwajibikaji katika sekta ya umma kwa manufaa ya umma.BASHE

”Mwalimu Nyerere mwaka 1975 aliwaambia wafanyakazi utii ukizidi unakuwa uoga na siku zote uoga huzaa unafiki na unafiki huzaa kujipendekeza na hivyo huzaa mauti”- Amesema Bashe.

”mwalimu akazidi kuwaambia wafanyakazi kama nyie watumishi wa umma kwa wingi wenu mmeshindwa kupiga kura ya kuwaondoa viongozi dhalimu ni bora mfe”-Amesema Bashe

”Na sisi kama CCM kwa wingi wetu tunashindwa kuishauri serikali kwa ukweli hatuna sababu ya kubaki kuwa madarakan nayasema haya kwa moyo mweupe nikiwa mwanachama wa CCM”-Amesisitiza Bashe.

Aidha Bashe amewasihi mawaziri kuunganisha nguvu ya pamoja katika kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji kwa manufaa ya wananchi kuliko kuachiana kazi hiyo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top