Loading...

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI KIBOKO AFANYA TUKIO HILI ZITO LA MWAKA NA KUMPIKU RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE...HII KWELI NI HISTORIA NA MAAJABU YA AINA YAKE

Dk. John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia mamia ya Wafanyakazi kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi (Mei mosi) mjini Dodoma
RAIS John Magufuli amempiku Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete katika kushusha kiwango cha makato ya kodi za mishahara kutoka asilimia 11 aliyoiacha (Kikwete) na kuwa asilimia 9, anaandika Hamisi Mguta.
Kwa muda mrefu wafanyakazi nchini walikuwa wakilalamikia kiwango kikubwa cha makato ya kodi kwenye mishahara yao ambapo Rais Kikwete aliahidi kupunguza zaidi lakini hakufikia kiwango cha sasa.
Mpaka anaondoka madarakani tarehe 5 Novemba  mwaka jana, Rais Kikwete aliacha makato hayo kuwa asilimi 11 ya mshahara. Hata hivyo ilielezwa kuwa, sababu kubwa ilitokana na Serikali ya Kikwete kutokuwa bunifu katika kutambua vyanzo vipya vya kodi, kuwepo kwa idadi kubwa ya wakwepa kodi pia vitendo vya rushwa na ufisadi kutamalaki.
Rais Magufuli ametoa punguzo hilo leo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo, amesema serikali yake imeamua kufikia uamuzi huo ili kuwapunguzia mzigo wafanyakazi kwani ndio kundi ambalo hawawezi kukwepa kulipa kodi.
“Watu ambao hawawezi kukwepa kulipa kodi ni wafanyakazi, ndiyo maana Serikali imeamua kupunguza mzigo huu,
“Haiwezekani mtu mwengine apate mshahara Sh. 30 milioni na mwengine apate 3,000,000 wakati anayepokea pesa ndogo ndiye anayefanyakazi kubwa, sina wivu na wanaopata mishahara mikubwa lakini nataka tunapopanda tupande wote,” amesema.
Amesema pamoja na uamuzi huo wa Serikali kupunguza makato ya kodi, ameahidi kuwa inampango wa kuongeza mishahara ili kuendelea kuwaletea nafuu wafanyakazi wanaojituma.

Amewataka wafanyakazi kupuuza wanaosema kuwa Serikali ya awamu ya tano haiwajali wafanyakazi kwani wanaosema hivyo wengi wao ndiyo wabadhilifu wanaoirudisha nyuma nchi.
“Serikali ya awamu ya tano haitambagua mfanyakazi wa aina yoyote anayefanyakazi kwa weledi,” amesema.
Hata hivyo Rais Magufuli amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa kuweka mfumo wa mishahara kuzingatia vigezo vya uzito wa kazi kwa misingi ya haki na usawa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top