Breaking News niliyopokea muda mfupi uliopita inahusu ajali iliyotokea Pwani ambapo watu wanne wamefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa katika ajali iliyohusika msafara wa kamati ya Tamisemi – Pwani
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo akizungumza na ITV kwa kile kilichotokea katika eneo hilo la tukio amesema…
>>>’Ni maeneo ya hapa Pwani tunatokea mafinga tulikuwa na kamati ya Tamisemi ambapo kwa kawaida kipindi hiki tunakagua miradi yetu sasa tulienda kukagua mradi wa maji na tulikuwa tunaelekea Yombo kukagua mradi, njiani tukawa tumepata ajali baada ya lori kugonga magari manne yaliyokuwa katika msafara wetu na kupelekea vifo vya watu wanne na majeruhi sita ambao wamekimbizwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kupatiwa huduma ya kwanza‘.
Post a Comment