Watu wa Ireland wanaadhimisha mwamko wa Pasaka 'Easter Rising',uliotokea karne moja iliyopita, iliyomaliza utawala wa Uingereza katika nchi hiyo.
Gwaride maalumu inafanywa katika mji mkuu wa jamhuri ya Ireland, Dublin, na maelfu ya watu wamesimama mabarabarani kutazama wanajeshi, wa sasa na waliostaafu, wakielekea Posta Kuu, ambapo mwamko huo ulianza na kumalizika.
Muammko huo uliyotokea 1916 ulipelekea kuundwa kwa Jamhuri ya Ireland.
Tangazo la kuundwa kwa taifa huru lilisomwa upya katika maadhimisho maalum nje ya jengo la Posta Kuu.
Viongozi wa muamko huo walijisalimisha kwa utawala siku tano baadaye baada ya mashambulio makali kutoka kwa majeshi ya Uingereza.
Waziri mkuu wa Ireland Kaskazini ambayo ni sehemu ya Uingereza alikataa kujiunga na maadhimisho hayo ya miaka mia moja 100 tangu vita vya uhuru kutoka kwa ukoloni wa Muingereza kuanza.
Waziri huyo anasema kuwa muamko huo ndio uliochochea machafuko yaliyotokea kati ya miaka ya 1970 na 1980.
Post a Comment