AMA kweli! Ng’ombe hazeeki maini, hivyo ndivyo walivyodhihirisha wasanii wakongwe wa Muziki wa Bongo Fleva mara baada ya kuporomosha bonge la shoo katika Mkesha wa Sikukuu ya Pasaka.
Mkesha huo ulifanyika jana usiku, katika Ufukwe wa Sunrise uliopo Kigamboni jijini Dar uliendana na sherehe ya kutimiza miaka 25 ya promota maarufu nchini, Majid Mdoe ‘Promota Bonga’ . Huku wasaniii kama Afande Sele, Dully Sykes, Jaffarai, Suma G, Manzese Crew, Mabaga Fresh, Zig Zag Crew, Fanani wa Hard Blastaz Crew, Soggy Dog, Inspectour Haruni ‘Babu’ Juma Nature, Sister P, Sold Ground Family Feruzi, Rich One na wengine kibao wakiwakumbusha mashabiki wao kwa muziki uliowahi kufanya vizuri kipindi cha nyuma.
Shoo hiyo iliandaliwa na na mmoja wa mapromota wakongwe wa muziki huo, Promota Bonga akishirikiana na Kituo cha Redio cha Times FM kilichopo Kawe jijini Dar
Post a Comment