SAID Chitembwe, Jaji nchini Kenya amemwacha huru Martin Charo aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kubaka mtoto wa mika 13.
Chitembwe amesema, mtoto huyo alijifanya ni mtu mzima na kufurahia kufanya tendo hilo hivyo haiwezi kuwa kesi ya kubaka licha ya Sheria ya Kenya kutambua mtoto huyo kuwa na umri wa miaka 18.
Hata hivyo jaji huyo amesema, ingawa umma utakasirishwa kwa mtu mzima kujihusisha na mapenzi na mtoto amesema, mambo ya mebadilika na kwamba watoto siku hizi wana shiriki ngono katika umri mdogo.
Vincent Monda, Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai nchini humo (DPP) amesema kuwa, hakufurahishwa na uamuzi wa Jaji Chitembwe katika mahakama ya rufaa kwa kumwacha na kwamba ofisi hiyo itakata rufaa dhidi ya jaji huyo.
Post a Comment