Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea Aprili 22 baada ya wahudumu wa nyumba ya wageni ya Sayari kubaini maiti katika chumba namba mbili.
Inadawa Aprili 20 mwanamke huyo akiwa na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi, walifika kwenye nyumba hiyo na kuchukua chumba kimoja wakisema wao ni wafanyabiashara wa mazao.
“Mwili wa marehemu uligundulika ukiwa kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Sayari chumba namba mbili saa 11 jioni na ulipochunguzwa ikagundulika kuwa kifo kilisababishwa maumivu ya jereha,”alisema Matei.
Mwanamke huyo alikuwa na jeraha kushoto mwa bega lake lililotokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali
Matei alisema kwa taarifa walizozipata bila shaka kijana aliyekuwa naye anahusika na mauaji hayo.
Wakati huo huo, jeshi la polisi wilayani Kilosa limemkamata Rogasian Jeremia kwa tuhuma za kumshambulia mkewe, Faustina Sizayi(25) kwa kumkatataka kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa anajihusisha na kazi ya ulinzi wa maduka baada ya polisi kumsaka kwa muda mrefu na ndipo Aprili 24 alikamatwa baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Post a Comment