Tumekuwa tukilalamikia uwezo wa wabunge wengi wa CCM kifikra. Bungeni ndipo mahala ambapo wahusika wanatakiwa kutuliza akili na kutoa mawazo chanya ya kulijenga taifa na kusimamia serikali katika majukumu yake ya kila siku. Mimi binafsi nimekuwa siioni faida ya wabunge zaidi ya asilimia 98 ya wabunge wa CCM kwa taifa! Ni mzigo ambao watanzania tunaubeba huku ukiwa hauna faida yoyote ile kwetu.
Mbunge wa Geita vijijini ndugu Joseph Kasheku Msukuma (CCM) amesema kuwa amefurahi sana bunge kutokuonyeshwa "live" kwa madai kuwa jimbo lake halina umeme hivyo watu wa jimbo hilo walikuwa wakilazimika kununua mafuta ya petrol kwa ajili ya jenereta ili kuangalia bunge "live". Aidha amesema kuwa kwa sasa wananchi hao hawatalazimika tena kuingia gharama ya mafuta hayo ya petrol na badala yake watajikita kwenye kilimo.
"Jimbo langu halina umeme, wananchi wangu walikuwa wakilazimika kununua mafuta yapetrol kwa ajili ya kuendesha jenereta ili waone bunge "live" hivyo walikuwa wanaingia hasara. Kwa sasa nimefurahi sana bunge kutokuonyeshwa "live" kwa kuwa hawatalazimika tena kuingia gharama ya kununua mafuta ya petrol! Watajikita zaidi kulima mashamba yao" alisema mbunge Msukuma.
Hao ndiyo wabunge wetu watukufu wa CCM wanaotakiwa kumshauri rais Magufuli anayetokana na chama chao.
Post a Comment