Loading...

Namuona Mwanamuziki Harmonize Ndani ya Diamond Platnumz


Moyowe ya Afande Sele akiwa na Jay mo moja kati ya nyimbo zangu chache ambazo huzisikiliza mara nyingi kwa siku. Moja ya kati ya maneno yenye busara aliyosema Afande Sele ni “Hii ni fani na msanii na msanii siko mwenyewe ili nifanikiwe inahitaji nikosolewe na inapobidi nisifiwe”

Kwa wafuatiliaji wa muziki hakika Harmonize si jina jipya katika masikio yao, Aiyola ni wimbo wake uliomtambulisha kwenye ramani ya bongo fleva yani muziki wa kizazi kipya mwaka 2015. Aiyola ni wimbo ulifanyika katika studio za WCB ambazo zipo chini ya msanii Diamond Platnumz ambapo Rich Mavoko na Ray Vanny ni miongoni mwa wasanii waliopo chini ya Label hiyo ya WCB.

Inadhihirika katika maisha ya binadamu kabla ya kutokea chochote basi lazima kuwe na ishara yoyote ile, kabla ya kutoka kwa Harmonize hakika ishara zilikuwepo hasa kwa wale wanatumiaji mtandao wa picha Instagram. Tulipata kuona tambo za msanii Diamond pamoja na wapambe wake wakiwa wanampamba na kumnadi msanii huyu chipukizi Harmonize.

Sikuwa na shaka kabla ya kumsikia na hata baada ya kumsikia, licha ya kuona maoni mengi kutoka kwenye team zilizopo katika mtandao wa picha wa Instagram. Maoni mengi yalikuwa na kusema jamaa anamuiga Diamond Platnumz.

Haikuwa rahisi kukubali kile ambacho walikuwa wanasema, bali nilifikiri ni chuki zilizopo katika hizi team ambazo kiundani hazina maana yoyote zaidi ya kutumia muda mwingi katika msanii pinzania na kushindwa kujenga hoja kwa msanii wao ili aweze kufanikiwa zaidi. Lakini wao huwa kinyume na zaidi wamelala upande wa lugha chafu na kudharirishana tu.

Waswahili husema “Lisemwalo lipo na kama lipo laja” Sikuwa mbinafsi katika kujipa muda na kuendelea kusikiliza wimbo wa aiyola, si jambo la kupinga mfanano ulikuwa na mdogo, ila ambacho nilihisi ni labda kipindi anafanya wimbo huu ushauri wa msanii Diamond ulihusika kwa 100%. (Hisia)

Bado ni wimbo wake mpya msanii chipukizi Harmonize aliyomshirkisha Diamond Platnumz, ambapo kwa sasa ni wimbo wa bado ndiyo wimbo unaongoza kuchezwa kwenye vituo vya radio na runinga Tanzania. Hii ni kwa mujibu wa Copyrights Management East Africa (CMEA)

Ishara za Harmonize kuwa ndani ya Diamond zimeonekana dhahiri katika wimbo huu wa bado. Hakika ameshindwa kuwa yeye imenichukua muda kidogo kufikiri kwanini ameamua kuwa Diamond?. Mara kadhaa nilipata wasaa wa kumsikiliza katika mahojiano kadhaa ambapo alisema “Diamond ndiye msanii ninaye mkubali kuliko yoyote yule”. Hivyo katika hilo ni wazi yeye ni shabiki wa Diamond licha ya kuwa bosi wake. Si jambo baya hakika ni jambo jema kufanya kazi na mtu ambaye unamkubali na kumpenda.

Lakini jambo la kufanya kile anachofanya Diamond hakika si jambo jema, ni wazi kama ni mwandishi au mdau mwenye mapenzi na muziki wa kizazi kipya basi hutoacha kusema ili kusaidia muziki kwa ujumla au kumsaidia Harmonize. Ni wiki kadhaa zimepita tangu kumuona msanii chipukizi Harmonize katika mahojiano ya kipindi cha runinga. Hakika nilimuona Harmonize ndani ya Diamond kwa mara nyingine tena , ila hii ilikuwa katika muoenekano wake hususani katika uchezaji,maringo na hata katika uongeaji.Ni wazi alishindwa kujizuia katika ule upande wa kumuiga Diamond, pia hata katika tumbuizo fupi alilofanya pale kwenye kipindi ni wazi nilimuona Diamond ndani yake.

Kuiga ni kitu pekee kinachoanguasha walio wengi katika mambo mengi ya kidunia. Leo hii unapomuiga msanii Diamond ni ngumu kuwa kama yeye maana ni tayari yeye ameshakuwa yeye, pia si rahisi kupenya katika sehemu nyingi maana tayari yeye yupo. Hii si kwa Diamond pekee bali kwa msanii yoyote yule.

Wasanii walio wengi hawajui madhara ya kumuiga msanii mwingine, na makosa mengi yanafanyika sababu hawajui kuna mahala watakwama.

Nadhani huu ni muda mzuri wa msanii chipukizi Harmonize kuchukua nafasi ya kufanya marekebisho katika muziki wake, na kutengeneza mbinu zake kama si sauti tu pekee na hata kuwa yeye zaidi ni vyema kumuacha Diamond na muziki wake.

Pia tusione ukweli kama ni ubaya kwenye maisha yetu ya kila siku, hakika tukikubali ile kweli basi tutakuwa wakweli kwenye kile ambacho utakuwa unafanya kila leo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top