Loading...

WANAOMKEJELI JPM WACHUNGUZWE

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rorya mkoani Mara kimesema watu wanaokejeli juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli si wazalendo , wanapaswa kuchunguzwa na Serikali.MAGUMwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Samwel Kiboye alisema hayo jana jijini Mwanza alipokuwa akizungumzia juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli kuchukua hatua dhidi ya watu wanaoiba fedha za umma.

“Kumeibuka tabia chafu kutoka kwa baadhi ya watu nchini kwa sasa, wanapotosha wananchi juu ya kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli katika kuwashughulikia mafisadi na wanaoiba rasilimali za nchi, ”alisema.

Alisema taifa haliwezi kukubali kuona kazi nzuri inayofanywa na Rais ikipotoshwa na watu wachache aliosema hawaitakii mema nchi. “Nani haoni kazi kubwa inayofanywa na Rais …, ameimarisha ukusanyaji wa mapato na ameboresha sekta ya afya, miundombinu, hivi watu hawa wanataka Rais awafanyie nini?,” alihoji na kuongeza:

“Ni aibu kuona watu wanahoji mambo ambayo hata kwa mtu ambaye hakwenda shule anaona mafanikio makubwa aliyofanya Rais Magufuli katika kipindi kifupi ambacho amekuwa madarakani.”

“Huko nyuma walikuwa wanamlaumu aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete kuwa alikuwa mpole, leo tumempata Rais anayesimamia ukuaji wa uchumi wa nchi wanaleta siasa, sisi Rorya tunasema tuko imara na tutakufa na Rais Magufuli”.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright NEWZ | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top