Loading...
Home »
Unlabelled »
ATLETICO MADRID WATANGULIA FAINALI
Ni shabiki gani wa mpira ambaye usingependa kumuona Diego Simeone akifundisha timu unayoishabikia? Arsenal,Manchester United,Chelsea wote wanalia makocha wao wabovu,Simeone sio muumini wa mpira mzuri bali muumini wa matokeo uwanjani pamoja na vituko vyake watu huachwa hoi sana na wanafurahishwa naye. Katika utawala wake wa kuifundisha Atletico Madrid anaingia fainali ya Uefa kwa mara ya pili.
MCHEZO WA NUSU FAINALI
Mchezo ulikuwa mzuri na wa kueleweka ule undava ambao ana ufanya akicheza na Real Madrid kidogo umepungua mpira umewekwa chini na ukachezwa japo uwanja ulikuwa umeinamia kwa Atletico Madrid,lakini Diego Godin na Juafran walisimama kuwazuia Frank Ribery,Douglas Costa pomoja na Robert Lewandowski ama kwa hakika walijitahidi sana kwa mchezo ule kama Bayern angekutana na ukuta wa timu ya England ule utani anaotaniwa Arsenal wakumuita Arse8 ungetokea jana umoja na nguvu ndiyo ulioifanya Atletico kuvuka hatua inayofuata.
VITUKO
Mchezo ulikuwa wa ‘Pressure’ kubwa kila mmoja akitaka ushindi wa haraka wakati Diego Simione akitaka kubadili mchezaji mwamuzi wa akiba alichelewesha kuwasiliana na mwamuzi mkuu wa ndani ya uwanja kilicho tokea Simeone alimchapa kofi kutokana na mzuka wa mechi uliokuwa umempanda. Na hili tatizo la makocha vijana,wakati simeone akiwa hajaishiwa na vituko naye Pep Guardiola uzalendo ulimshinda alionekana mda wote ametoka katika eneo lake na kuingia hadi uwanjani kabisa akitoa maelekezo na wakati mwingine akipaniki alionekana akitaka kupambana na Simeone au labda aliogopa ahadi yake kuwa endapo angetolewa na Atletico wamuue?
MATOKEO
Bayern imeshinda magoli 2-1 Xabi Alonso DK 31 na Lewandowski DK 74 huku Muller akikosa penati na lile la Atletico lilipatikana dakika ya 54 kupitia kwa Greizmann wakati Torres naye alikosa tuta. Kwa sheria ya UEFA na sheria ya goli la ugenini inaipeleka Atletico moja moja Fainali ya michuano hii mikubwa na yenye msisimko duniani.
Wednesday, 4 May 2016
Post a Comment