Loading...
Home »
Unlabelled »
CCM YAENDELEZA USHINDI KESI ZA UCHAGUZI
Baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana uliohusisha Wabunge, Madiwani na Rais, wagombea mbalimbali ambao hawakuridhishwa na Matokeo ya Uchaguzi waliamua kufungua kesi kupinga ushindi kwa wabunge waliotangazwa kuibuka kidedea.
Miongoni mwa waliofanya hivyo ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje (Chadema) dhidi ya Mbunge wa sasa Stanslaus Mabula (CCM), Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR- Mageuzi) dhidi ya mbunge wa sasa Husna Mwilima (CCM) pamoja na Willy Mungai (Chadema) dhidi ya Mbunge wa sasa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi.
Katika kesi hizo ambazo mbili zimekwishatolewa hukumu Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuibuka mshindi kupitia kwa wabunge wake katika majimbo ya Nyamagana na Mafinga.
Leo Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetoa hukumu na kumpa ushindi Mbunge wa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi kufuatia kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo hilo kupitia Chadema Willy Mungai.
Mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo Chumi akasema “ Ninawaomba wenzetu Chadema wasifikire kukata rufaa kuendelea na kesi hii kwani katika hoja zao zilizopelekea kwenda mahakamani ufafanuzi umetolewa vizuri na jaji hivyo kuendelea kukata rufaa ni kuendelea kuwacheleweshea wananchi wa Jimbo la Mafinga kupata maendeleo”.
Wednesday, 4 May 2016
Post a Comment