Loading...
Home
»
NEWS
»
BREAKING NEWS: MSEMAJI ASIE KAUKIWA NA MATUKIO WA CCM OLE SENDEKA AZUA GUMZO NA KUCHAFUA HALI HEWA KABISA NDANI YA CHAMA CHAKE BAADA YAKUTOA KAULI HII KWA VIONGOZI HAWA NI SINTOFAHAMU IMETAWALA SASA CCM NI TUMBO JOTO
Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa! Kile kilichokuwa kikisubiriwa na wengi hatimaye kimeanza kuonesha dalili za kutimia baada ya Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ole Sendeka kuweka bayana kuwa chama chake kipo katika hatua za mwisho za makabidhiano ya nafasi ya Uenyekiti wa Taifa kati ya Mwenyekiti wa sasa, Jakaya Kikwete na Rais Dk. John Magufuli.
Swali linalogonga vichwa vya Watanzania walio wengi na wafuasi wa chama hicho ni Rais Magufuli ataweza kuisafisha CCM dhidi wa mafisadi kama anavyofanya hivi sasa kwa Taifa la Tanzania dhidi ya walioitafuna nchi na kuneemeka kwa kipindi kirefu?
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe hivi karibuni amenukuliwa akisema Rais Magufuli anatumbua majipu pasipo kugusa kiini; miongoni mwa maswali yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi ni vigogo na mizizi iliyopandikizwa ndani ya CCM kwa kipindi kirefu Rais Magufuli ataweza kukabiliana nao ili kuiacha safi CCM 2020?
Dk. Jakaya Kikwete anatazamiwa wakati wowote kumkabidhi Rais Dk. Magufuli kijiti cha Uenyekiti wa chama hicho huku kauli, maamuzi na misimamo ya Rais Magufuli vikitajwa kuwa mwiba mkali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), je ataweza kuiponya CCM kwa rungu atakalokabidhiwa?
Filed Under:
NEWS
Wednesday, 4 May 2016
Post a Comment